Wanafunzi walionekana kunyeshewa wakienda shuleni wapata ufadhili wa masomo (video)

Shirika hilo liliwaomba wananchi kujitokeza kutoa ufadhili wowote ili kuwasaidia watoto hawa ndoto yao ya masomo isife.

Muhtasari

• Wanafunzi hao walikuwa wanatembea kwa mvua bila sweta wala mwavuli.

• Kampuni hiyo iliahidi kuwatafutia shule bora ambayo wangesomea ili ndoto ya elimu yao isipotee.

Video ilinosambaa ya wanafunzi wawili wasichana waliokuwa wakitembea wakiwa wananyeshewa imegusa mioyo za wanamitandao pamoja na kampuni mmoja ya kuuza viatu.

Wasichana hao walikuwa wanapita kando ya barabara kuu huku mvua kali ikiwa inawanyea bila hata sweta, mwavuli au kitu kizito kinachoweza kuwakinga dhidi ya baridi kali iliyokuwa inawakeketa.

Mmoja alitembea miguu tupu huku akiwa amebeba viatu vyake, huku mwingine akifuata kwa karibu kwa nyuma.

Kampuni hiyo Bravo Shoes Community Support  iliyoko Kampala, Uganda ilionekana kuwahurumia watoto hao waliokuwa hawajali mazingira wanamotembelea barabarani masaa ya asubuhi au kasi ya magari yaliokuwa yanapita kwa ajili ya ari waliokuwa nayo ya kutaka kufika shuleni mapema.

"Upendo wa elimu! Walivumilia mvua hadi wakafika shuleni, ambayo ilionekana kuwa mbali," kampuni ya Bravo Shoes Community Support ilisema kwenye ukurasa wao wa twitter.

''Tunawatafia shule bora zaidi ili ndoto na upendo wao kwa elimu isipotee!'' Kampuni hiyo ilizidi kusimulia.

''Nawaombea mema katika ufanisi wao''  naye Lusanda mmoja wa wanamitandao aliwatakia heri.

Shirika hilo lenye azimio la kuboresha maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira duni, lilitoa wito kwa wananchi kuwasaidia kuwatafuta wasichana hao wawili na kuwasaidia.