FIDA kuisaidia familia ya mwanafunzi aliyeuwawa na polisi kutafuta haki

FIDA ilisema itaisaidia familia katika harakati zao za kutafuta haki kwa kifo cha mwanao.

Muhtasari

• FIDA ilisema itaisaidia familia katika harakati zao za kutafuta haki kwa kifo cha mwanao.

Bunduki
Bunduki
Image: Andrew Kasuku

Shirikisho ya wanasheria wanawake nchini FIDA limelaani vikali mauaji ya mwanafunzi wa kike aliyepigwa risasi na polisi mjini Kisumu siku ya Jumanne.

FIDA,katika taarifa kwa vyombo vya Habari ilisema mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Upili ya mseto ya Simero ni ya kusikitisha.

“Tunalaani kitendo hicho kiovu kwa maneno makali iwezekanavyo," taarifa za FIDA ilisema.

Jecinta Achieng mwenye umri wa miaka 19 alipigwa risasi na polisi siku ya Jumanne asubuhi akiwa amebebwa kwenye pikipiki. Kulingana na wazazi wake Achieng alikuwa ameenda kununua bidhaa za kwenda nazo shuleni tayari kwa muhula wa pili.  

FIDA ilisema itaisaidia familia katika harakati zao za kutafuta haki kwa kifo cha mwanao.Pia waliilaani tukio hilo.

Walitoa wito kwa Mamlaka Huru ya Kusimamia shughuli za Polisi (IPOA) kufanya uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusu mauaji ya Achieng.

Achieng ambaye aliaga kabla ya kufika hopitali alikuwa miongoni mwa watu wanne waliopata majeraha ya risasi wakati polisi walipofyatulia risasi umati wa  wakati maafisa wa polisi walipokuwa wakifuata matatu kwa kutosimama katika kizuizi. 

"Binti huyo aliletwa hospitalini na tulipomchunguza, tuligundua kuwa tayari alikuwa amefariki kutokana na jeraha la risasi," mkurugenzi wa hopitali ya Agha Khan daktari Eshiwani alisema.

FIDA wakati huo huo imewataka polisi kujiuzuia na kuacha kutumia risasi kila wakati kuna changamoto kiasi. “Tunasalia na wasiwasi kuhusu visa vinavyoongezeka vya utumizi mbaya wa bunduki na mauaji nchini.”