Rais Ruto afanya mabadiliko ya makatibu

Harry Kimtai alijiunga na Wizara ya Afya, baada ya kuhudumu kama PS wa Mifugo katika Wizara ya Kilimo.

Muhtasari
  • Katika taarifa iliyotiwa saini na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, Peter Kiplagat Tum alihamshwa tena kutoka Wizara ya Afya hadi Wizara ya Michezo.
Rais William Ruto
Rais William Ruto
Image: Facebook

Rais William Ruto, mnamo Jumanne, Mei 16, aliwateua tena Makatibu Wakuu saba kama sehemu ya kupanga upya serikali.

Ruto aliteua makatibu wawili wapya katika Wizara ya Afya, baada ya kumfuta kazi Waziri wa Afya Dkt Josephine Mburu na kumteua tena Peter Kiplagat Tum.

Katika taarifa iliyotiwa saini na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, Peter Kiplagat Tum alihamshwa tena kutoka Wizara ya Afya hadi Wizara ya Michezo.

Harry Kimtai alijiunga na Wizara ya Afya, baada ya kuhudumu kama PS wa Mifugo katika Wizara ya Kilimo.

Marry Muthoni Muriuki atahudumu kama PS Afya ya Umma na Viwango vya Kitaalamu katika Wizara ya Afya, aliyehamishwa kutoka Mambo ya Ndani, ambako aliongoza Huduma za Urekebishaji.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Misitu Ephantus Kimani alihamishwa kutoka Wizara ya Kilimo hadi Wizara ya Umwagiliaji kama Waziri wa Maji.

Jonathan Mueke alihamishwa kutoka Michezo hadi Wizara ya Kilimo.

Ruto alimteua Gitonga Mugambi kama katibu wa mzingira.

Ili kuwezesha kubadilishwa kwa nafasi hiyo ndani ya safu ya makatibu wakuu, rais alimteua Faith Njeri kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Usimamizi wa Utendakazi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri.