'Sihitaji nyongeza ya mshahara,'Ledama asema kuhusu pendekezo la SRC

Mshahara wa Naibu Rais Rigathi Gachagua utaongezeka kutoka Sh1,227,188 za sasa hadi Sh1,367,438.

Muhtasari
  • Katika taarifa, seneta huyo wa Narok alisema hahitaji nyongeza ya mshahara ilhali hakuna anayewabana watu anaowawakilisha.
LEDAMA 2
LEDAMA 2

Seneta wa Narok Ledama Olekina amejibu mapitio ya Tume ya Mishahara na Marupurupu ambayo yatashuhudia maafisa wa serikali wakipata nyongeza ya mishahara ya asilimia 14.

Kulingana na SRC, nyongeza hiyo itawaepusha na gharama ya juu ya maisha.

Katika taarifa, seneta huyo wa Narok alisema hahitaji nyongeza ya mshahara ilhali hakuna anayewabana watu anaowawakilisha.

Alisisitiza kuwa SRC inahitaji kusitisha ukaguzi huo.

Ledama alisema kinachotakiwa kufanywa ni serikali ipunguze ushuru unaotozwa watu wa Kenya.

"Sihitaji nyongeza ya mshahara ili kunipunguzia gharama ya juu ya maisha huku watu ninaowawakilisha hakuna anayewapunguzia ... tafadhali punguza ushuru! @srckenya acha!" alisema.

Katika ukaguzi huo, SRC inapendekeza kwamba Rais, naibu wake, makatibu wa Baraza la Mawaziri na wabunge miongoni mwa maafisa wengine wa serikali.

Iwapo itaidhinishwa, mshahara wa Rais utaongezeka kutoka Sh1,443,750 hadi Sh1,546,875 kufikia Julai 1, 2023.

Mshahara wa Naibu Rais Rigathi Gachagua utaongezeka kutoka Sh1,227,188 za sasa hadi Sh1,367,438.