Ndoto yangu inatimia-Faith Kipyegon asema

Kipyegon aliapa kuendelea kujitutumua katika siku zijazo.

Muhtasari
  • Msichana huyo mwenye umri wa miaka 29 alijitolea muda wake na akapata ushindi katika dakika 14 kwa sekunde 53.88.
Faith Kipyegon
Faith Kipyegon
Image: HISANI

Faith Kipyegon Jumapili alizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kushinda dhahabu yake ya pili katika mji mkuu wa Hungary.

Siku ya Jumamosi, Kipyegon alisisitiza hadhi yake kama mmoja wa magwiji wa muda wote kwa kutinga mbio za kihistoria za mita 1,500/5,000 katika Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Budapest.

Baada ya kushinda taji la tatu la dunia la mbio za mita 1,500 siku ya Jumanne, Kipyegon aliwasilisha kiwango kingine cha ubora, wakati huu katika mbio za mita 5,000, na kushinda dhahabu yake ya pili katika mji mkuu wa Hungary.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 29 alijitolea muda wake na akapata ushindi katika dakika 14 kwa sekunde 53.88.

Katika taarifa Jumapili, Kipyegon alisema kuwa alikuwa akiishi msimu wake.

"Huu umekuwa mwaka wa ajabu kwangu. Kuweka historia jana, kushinda medali mbili za dhahabu katika michuano ndio nilikuwa nikitamani msimu huu," alisema.

"Ndoto yangu ilitimia, inashangaza. Nimekuwa thabiti, nikizingatia mstari wa kumaliza na kuandika historia," Kipyegon aliongeza.

Kipyegon aliapa kuendelea kujitutumua katika siku zijazo.

Alitoa shukrani kwa Wakenya kwa kumpa usaidizi, haswa bintiye.

"Binti yangu ananipa sapoti ya ajabu, huwa ananiambia naweza kufanya hivyo. Mwisho kabisa, nataka kuishukuru timu yangu ya ajabu, kocha wangu, usimamizi wangu na mashabiki wote wa ajabu!" Kipyegon aliongeza.

Kufuatia ushindi wake, Rais William Ruto alimtaja Kipyegon kama binti mahiri wa udongo.

"Faith Kipyegon mwenye kipaji, wa kipekee na asiye na kifani ameshinda medali ya pili ya Dhahabu katika mbio za mita 5000 kwenye Riadha za Dunia huko Budapest," aliongeza.

Naibu Rais Rigathi Gachagua alitaja Kipyegon kama fahari ya Kenya.