Midoli ya kufanya mapenzi, dawa za Viagra miongoni mwa vitu vilivyonaswa JKIA

Mamlaka hiyo ilifanikisha kunasa bidhaa hizo ambazo ni pamoja na midoli ya kufanya mapenzi 14,pakiti 24 za dawa ya kuongeza nguvu za kiume, Viagra, pakiti za shisha miongoni mwa vingine.

Muhtasari

• Bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na drone 339, bunduki 7, bunduki 18 za kuchezea, risasi 11, pingu 8, Walkie talkies 24, pakiti 24 za viagra.

• Nyingine ni; toys 14 za ngono, 58 za shisha na krimu 60 za kupaka rangi.

Midoli ya mapenzi uanaswa JKIA. Image: HISANI
Midoli ya mapenzi uanaswa JKIA. Image: HISANI

Maafisa wa KRA katika uwanja wa ndege wa JKIA walifanikiwa kunasa shehena ya vitu kadhaa ambavyo ilisema vilikuwa vinajaribishwa kuingizwa nchini kwa za kimagendo ili kukwepa ushuru.

Kwa mujibu wa picha na video ambazo zimeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, midoli kadhaa ya kufanya ngono, dawa za kuongeza nguvu za kiume, Viagra, ni miongoni mwa vitu vilivyonaswa.

Bidhaa hizo zilidaiwa kusafirishwa hadi nchini kati ya Julai na Oktoba 2023, maafisa wa KRA walisema. Mamlaka iliorodhesha angalau vitu 430 kama vizuizi huku 132 vikiwa vimepigwa marufuku.

Bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na drone 339, bunduki 7, bunduki 18 za kuchezea, risasi 11, pingu 8, Walkie talkies 24, pakiti 24 za viagra.

Nyingine ni; toys 14 za ngono, 58 za shisha na krimu 60 za kupaka rangi.

Kunaswa kwa bidhaa hizo kunajiri wakati ambapo serikali na mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA wameorodhesha mipango kabambe ya kuhakikisha kwamba mianya yote ya ukwepaji ushuru inazibwa ili kuhakikisha serikali inakusanya ushuru kwa njia zinazostahili na zinazofaa.