Thika: Vijana wenye tatoo wafungiwa nje ya zoezi la kuajiriwa kujiunga NYS

Wengine waliondolewa kwa sababu ya makosa katika vitambulisho vyao vya kitaifa, ambavyo vingi viliorodhesha mahali pa kuzaliwa kama kituo tofauti na kituo cha kuajiri.

Muhtasari

• Licha ya idadi kubwa ya vijana wa Thika, waliojitokeza walikuwa wachache.

•  Waliojitokeza walisema walifurahia fursa zilizowangoja baada ya mafunzo ya NYS.

Nyanya atishia kumpa mjukuu mwenye tattoo laana
Nyanya atishia kumpa mjukuu mwenye tattoo laana
Image: X

Huku zoezi la kuajiri vijana 15,000 kwa Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) ikiendelea kote nchini, baadhi ya vijana eneo la Thika, Kaunti ya Kiambu waliondolewa kwenye zoezi hilo kutokana na kujichora tattoo katika sehemu mbalimbali za miili yao, NTV Kenya iliripoti Jumanne.

Ingawa wengi wao walifaulu majaribio ya utimamu wa kiakademia na kimwili, baadaye walionekana kuwa hawastahiki kwa sababu ya usanii wao wa mwili.

Peterson Mwangi, mmoja wa wagombeaji waliofukuzwa, aliambia kituo hicho cha runinga kwamba anajuta kuwa na wino wa mwili kwa sababu ulimnyima fursa ya kujiunga na taasisi ya kijeshi.

Wengine waliondolewa kwa sababu ya makosa katika vitambulisho vyao vya kitaifa, ambavyo vingi viliorodhesha mahali pa kuzaliwa kama kituo tofauti na kituo cha kuajiri.

Licha ya idadi kubwa ya vijana wa Thika, waliojitokeza walikuwa wachache. Waliojitokeza walisema walifurahia fursa zilizowangoja baada ya mafunzo ya NYS.

 

Walisema walivutiwa na mafunzo hayo kutokana na agizo la Rais William Ruto kwamba Huduma ya Kitaifa ya Polisi, Vikosi vya Ulinzi vya Kenya, Huduma ya Wanyamapori ya Kenya na Huduma ya Misitu ya Kenya kuajiri asilimia 80 ya idadi yao kutoka NYS.

 

Zoezi la kuajiri NYS limekuwa likiendelea kote nchini tangu Jumatatu.