Taita Taveta: Mlezi achoma nyeti za mvulana wa miaka 6 kwa kukojoa kitandani

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka sita aliachwa chini ya uangalizi wa shangazi yake na binamu yake huku mama yake akikwenda Saudi Arabia kutafuta ajira.

Muhtasari

• Kulingana na ripoti ya polisi iliyoonwa na TV47, mshtakiwa aliyetambuliwa kama alidaiwa kumvamia binamu yake wa miaka 6 mnamo Ijumaa, Machi 29.

Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Image: Shutterstock

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 34 anashikiliwa na polisi kaitka kaunti ya Taita Taveta baada ya kudaiwa kuchoma nyeti za mtoto mvulana mwenye umri wa miaka 6 kisa kakojoa kitandani.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyoonwa na TV47, mshtakiwa aliyetambuliwa kama alidaiwa kumvamia binamu yake wa miaka 6 mnamo Ijumaa, Machi 29.

"Takriban saa 0700, binamu yake Zawadi mwenye umri wa miaka 34 alichoma sehemu zake za siri kwa kutumia karatasi zilizoungua kwa kukojoa katika kitanda chake.”

“Mtoto huyo alipata majeraha ya moto kwenye msingi wa uume wake,” ilisoma sehemu ya ripoti hiyo kama ilivyonukuliwa na TV47.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka sita aliachwa chini ya uangalizi wa shangazi yake na binamu yake huku mama yake akikwenda Saudi Arabia kutafuta ajira.

Baada ya tukio hilo, Zawadi aliongozana na kijana huyo hadi katika Zahanati ya Kikatoliki ya Tarasaa ambako alitibiwa na kuruhusiwa.

Mwathiriwa alirejelewa katika Hospitali ya Kaunti ndogo ya Ngao kwa uchunguzi zaidi ambapo pia walipata fomu ya P3.

Kesi hiyo iliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Tarasaa na mshukiwa alikamatwa. Zawadi atasalia chini ya ulinzi wa polisi hadi Jumanne wiki ijayo atakapofikishwa mahakamani.

Kisa hiki kinaripotiwa takribani wiki mbili baada ya kisa sawia kuripotiwa kaunti ya Meru ambapo mke wa askofu mmoja aliripotiwa kujeruhi nyeti za mvulana wa miaka 17 kwa kumshuku kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na binti yake wa miaka 15.