Oktoba 10: Iliyokuwa inaitwa Moi Dei yabadilishwa rasmi na kuitwa Mazingira Dei

Awali ilikuwa inaitwa Moi Dei lakini baada ya kurejeshwa na mahakama, baadhi walikuwa wanaiadhimisha Huduma dei huku wengine pia wakiita Utamaduni dei.

Muhtasari

• Siku hiyo ambayo ilikuwa imefutiliwa mbali kama siku ya kitaifa ilirudishwa tena na mahakama miaka michache iliyopita.

• Hata hivyo, haikubainishwa wazi kuhusu shughuli rasmi ya kiserikali ambayo inastahili kufanyika katika siku hiyo.

 

Image: PCS

Sasa ni rasmi sikukuu ya Oktoba 10 kila mwaka ambayo ilikuwa inakanganya kwa kuitwa Utamaduni dei, Moi dei na Huduma dei imebadilishwa na itakuwa inaitwa Mazingira Dei.

Hii ni baada ya rais Ruto kutia saini kuwa sheria muswada wa marekebisho wa mwaka 2024.

Siku hiyo sasa itakuwa inatumiwa na Wakenya wote kujukumika katika kutunza mazingira ikiwemo kuendesha shughuli za upanzi wa miti.

“Mswada huu unarekebisha kipengele cha siku za likizo za kitaifa ili kubadilisha Utamaduni dei kuwa Mazingira dei ambayo itakuwa inaadhimishwa Oktoba 10 kila mwaka. Hii inalenga kuwapa heko maafisa wa serikali kwa juhudi zao za kutunza mazingira,” sehemu ya ripoti ya PSC ilisoma kwa mujibu wa Nation.africa.

Itakumbukwa mwaka 2022 wakati wa kuapishwa kwake, rais Ruto alisema moja ya malengo yake makuu ifikapo mwaka 2032 ni kuhakikisha Kenya kumepandwa miti Zaidi ya bilioni 15.

Siku hiyo ambayo ilikuwa imefutiliwa mbali kama siku ya kitaifa ilirudishwa tena na mahakama miaka michache iliyopita.

Hata hivyo, haikubainishwa wazi kuhusu shughuli rasmi ya kiserikali ambayo inastahili kufanyika katika siku hiyo.

Awali ilikuwa inaitwa Moi Dei lakini baada ya kurejeshwa na mahakama, baadhi walikuwa wanaiadhimisha Huduma dei huku wengine pia wakiita Utamaduni dei.