Bangi yapatikana katika magunia manne ya maharage Moyale

Misokoto 22 ya bangi yenye thamani ya Kshs.435,000 ilipatikana ndani ya gunia hizo

Muhtasari

•Maafisa hao wanasemekana kutumia mbwa wa kunusa ambaye alitambua kitu cha kutiliwa shaka ndani ya magunia hayo.

• Misokoto 22 ya bangi yenye thamani ya Kshs.435,000  ilipatikana ndani ya gunia hizo.

Magunia yaliyonaswa na Maafisa wa upelelezi
Image: DCI X

Maafisa wa upelelezi katika Kaunti Ndogo ya Moyale walinasa dawa za kulevya zilizohifadhiwa kwenye magunia manne ya maharagwe Jumatatu kufuatia taarifa kutoka kwa umma.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilisema kwamba maafisa walipokea ripoti za "mtu anayeshukiwa na magunia manne ya maharagwe" katika kituo cha mabasi ya Liban na kusababisha jibu la haraka la polisi.

"Walipofika, waligundua kuwa magunia hayo yalikuwa yameachwa bila mtu yeyote kwenye lango la afisi hiyo  ya kukata tiketi, na mwenye nyumba hakupatikana, kwani alidaiwa kuwa alienda kutafuta karatasi za kuidhinishwa na ofisi ya KRA," DCI ilisema kwenye X.

Maafisa hao wanasemekana kutumia mbwa wa kunusa ambaye alitambua kitu cha kutiliwa shaka ndani ya magunia hayo.

Maafisa kisha walipeleka magunia hayo hadi afisi za DCI Moyale ambako yalifunguliwa, na kufichua misokoto 22 ya bangi yenye thamani ya Kshs.435,000.

Shehena hio inawekwa chini ya ulinzi hili kutumika kama ushahidi.

Wakati huo huo, msako mkali unaendelea kuwatafuta washukiwa.