Ruto yuko Murang'a, Mawaziri kuongoza upandaji miti katika kaunti

Naibu Rais Rigathi Gachagua atakuwa Samburu kwa shughuli inayolenga kuongeza eneo la misitu nchini kwa miti bilioni moja zaidi.

Muhtasari

Ratiba iliyoonekana na gazeti la Star inafichua kuwa kila mmoja wa mawaziri22 wa Baraza la Mawaziri ataongoza harakati za upandaji miti katika kaunti mbalimbali.

CSs pia wamepewa majukumu ya kufuatilia maendeleo ya miti ambayo ingepandwa katika kampeni ya kitaifa ya misitu.

Image: PCS

Rais William Ruto leo anatarajiwa kuongoza shughuli ya kitaifa ya upandaji miti kutoka kaunti ya Murang'a.

Naibu Rais Rigathi Gachagua atakuwa Samburu kwa shughuli inayolenga kuongeza eneo la misitu nchini kwa miti bilioni moja zaidi.

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi anatazamiwa kuongoza timu za Chogoria, kaunti ya Tharaka Nithi, akiandamana na viongozi wa eneo hilo.

Ratiba iliyoonekana na gazeti la Star inafichua kuwa kila mmoja wa mawaziri22 wa Baraza la Mawaziri ataongoza harakati za upandaji miti katika kaunti mbalimbali.

CSs pia wamepewa majukumu ya kufuatilia maendeleo ya miti ambayo ingepandwa katika kampeni ya kitaifa ya misitu.

Waziri wa Mazingira Soipan Tuya ataongoza kampeni hiyo huko Vihiga na Samburu na anatarajiwa kupanda miti milioni 6.5 mwishoni mwa kampeni.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ataongoza kampeni hiyo katika kaunti tano-Marsabit, Mandera, Turkana, Garissa na Wajir-, akilenga miti milioni 2.8.

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi ataongoza kampeni ya upandaji miti Makueni na Samburu, akilenga miti milioni mbili.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amepewa kaunti za Kilifi na Bungoma na ana kazi ya kupanda miti milioni moja.

Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria amepewa kaunti za Bungoma, Kisumu na Siaya, akilenga miti milioni 2.5.

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu ataongoza zoezi hilo katika Trans Nzoia na Migori (Msitu wa Migori) na lengo lake ni la miti milioni 2.7.

Eliud Owalo wa ICT amepewa kazi ya Nandi na Kisii ambapo anatarajiwa kupanda miti milioni moja.

Waziri wa Kazi Florence Bore anatazamiwa kuwa Bomet na Nyamira kwa kampeni hiyo na analengo la miti milioni moja.

Waziri wa Maji Zacharia Njeru anaelekea Kajiado na Kiambu kwa shughuli hiyo na analengo la miti milioni 1.8.

Alfred Mutua wa Utalii anatazamiwa kuongoza upandaji miti huko Kitui na Taita Taveta, akilenga miti milioni 2.8.

Waziri wa Uchumi wa Bluu Salim Mvurya ataongoza kampeni hiyo katika Tana River na Lamu, huku Waziri wa Jinsia Aisha Jumwa akisimamia Kakamega na Kwale.

Waziri wa ulinzi Aden Duale ametumwa katika kaunti za Isiolo na Nakuru na analengwa la miti milioni 2.8.

Mwenzake wa Barabara Kipchumba Murkomen atakuwa Homa Bay na Mombasa, ambapo juhudi zake ni kusaidia miti milioni 5.6 kukua.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amepewa Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi, lengo likiwa ni la milioni moja, huku Waziri wa Vyama vya Ushirika Simon Chelugui ataongoza kampeni katika Uasin Gishu na Murang'a.

Waziri wa Biashara Rebecca Miano atakuwa Embu na Narok ambapo anatarajiwa kuongoza upandaji na uhifadhi wa miti milioni moja.

Davis Chirchir wa Energy atakuwa katika kaunti za Kericho na Baringo, huku Njuguna Ndung’u wa Hazina akiwa Machakos na Nyandarua.

Waziri wa EAC Peninah Malonza ataongoza kampeni hiyo huko Meru na Busia, huku Waziri wa Ardhi Alice Wahome atakuwa Nyeri na Laikipia, lengo likiwa ni la miti milioni 2.7.