Tazama maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 16.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti 5 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Nairobi, Pokot Magharibi, Kisumu, Nyeri, na Laikipia.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 16.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Nairobi, Pokot Magharibi, Kisumu, Nyeri, na Laikipia.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za maeneo ya Parklands, Mutuini na Kabiria yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Ortum na Sigor katika kaunti ya Pokot Magharibi zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Obumba na hospitali ya Chiga katika kaunti ya Kisumu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, baadhi ya sehemu za maeneo ya Marua na Muruguru zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Mukima, Khe na Nyariginu katika kaunti ya Laikipia pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.