Cheruiyot Kirui: Mkenya aliyejaribu kukwea Mlima Everest bila kutumia oksijeni ya ziada apotea

Mlima Everest, unaotajwa kuwa mlima mrefu Zaidi duniani kwa urefu wa mita 8, 850 [sawa na futi 29, 035] unapatikana katika mpaka wa mataifa ya Nepal na Uchina.

Mlima Everest
Mlima Everest
Image: Hisani

Cheruiyot Kirui, Mkenya anayefanya kazi kwenye benki ambaye alikuwa katika ziara ya kuukwea mlima mrefu Zaidi duniani, Everest bila kutumia okisjeni ya ziada ameripotiwa kutoweka.

Mlima Everest, unaotajwa kuwa mlima mrefu Zaidi duniani kwa urefu wa mita 8, 850 [sawa na futi 29, 035] unapatikana katika mpaka wa mataifa ya Nepal na Uchina.

Kwa mujibu wa taarifa, Kirui, ambaye ni mfanyikazi wa benki ya KCB humu nchini alikuwa anatazamia kuweka rekodi ya kufika katika kilele cha mlima huo bila kutumia okisjeni ya ziada, katika jaribio lake la kuujaribu mwili wa kawaida wa binadamu.

Kampuni ya kuwasafirisha watalii katika mlima huo ilisema kwamba Cheruiyot na mwenzake ambaye walikuwa wamekwea hadi urefu wa mita 8,000 walitoweka huku mwingine raia wa Romania akiripotiwa kufariki katika Camp III.

Msimamizi wa kaouni hiyo ya kutembeza watalii kwa jina Mingma Sherpa aliambia vyombo vya habari kwamba Cheruiyot ambaye alitaka kukwea mlima huo bila kutumia okisjeni ya ziada alianza kuonyesha tabia za ajabu kabla ya kupoteza mawasiliano nao baada ya kukwea mita 8,000, akisalia na mita chache kufika kileleni.