KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo Jumamosi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Mei 25.

Muhtasari

•KPLC imetangaza baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, West Pokot na Nyeri.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Mei 25.

Katika taarifa ya siku ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, West Pokot na Nyeri.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za mtaa wa Westlands zikiwemo ABC Place, Manyani, Delloite, Westend Tower, sehemu za Waiyaki Way na viunga vyake zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za  eneo la Kapenguria katika kaunti ya West Pokot zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za mji wa Karatina katika kaunti ya Nyeri pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.