DCI wamkamata mshukiwa kwa wzizi wa vipuri vya magari Kiambu

Mhuni huyo amekuwa akiwasumbua wakaazi wa Kiamumbi wanaoegesha magari yao usiku,kwa muda mrefu.

Muhtasari

•Maafisa wa polisi wamemkamata mhuni mmoja eneo la Kiamumbi,kaunti ya Kiambu akiwa ameshikilia taa za mbele za gari.

•Francis Ndichu alikamatwa usiku wa Jumatano alipokuwa akijaribu kuvamia gari ili kuondoa vifaa  hivyo muhimu.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Maafisa wa polisi wamemkamata jamaa mmoja anayejishughulisha na wizi wa vifaaa muhimu vya magari eneo la Kiamumbi,kaunti ya Kiambu.

Baada ya kuwakosesha usingizi wakazi wa Kiamumbi kwa kuvamia  na kuharibu magari yao  yanayoegeshwa gizani, mshukiwa anayejulikana kama Francis Ndichu Kimani mwenye umri wa miaka 24, hatimaye amenaswa.

Maafisa wa DCI walifichua kuwa kukamatwa huko kulifuatia oparesheni kali iliyofanywa kwenye mtaa wa Santiago, eneo ambalo mara kwa mara hutembelewa na maadui wa maendeleo kiasi kwamba baadhi ya madereva wanaohofia uharibifu wa magari yao ama huyaacha mbali katika maeneo yanayodhaniwa kuwa ni salama.Madereva wengi hutumia fedha za ziada kwa walinzi au kulala kwenye magari ili kuyaangalia wenyewe.

Oparesheni hio ilitekelezwa usiku wa Jumatano huku maafisa wa polisi wakijiweka sawa katika maeneo tofauti.

Wakiongozwa na OCS wa eneo hilo, maafisa hao wa polisi walijizatiti usiku kucha, hadi saa 3:40 asubuhi wakati mwizi huyo alionekana akipanua ukuta wa majengo ya kuegesha magari.

Katika muda wa sekunde chache kabla ya kamanda huyo kuwaelekeza watu wake kwenye hatua inayofuata,Mshukiwa huyo alikamatwa akiwa ameshikilia gridi ya mbele na taa ya mbele ya gari aina ya Toyota Harrier, lililotolewa kwa ustadi kwenye gari la familia ya mwenye nyumba.

"...sehemu za gari zilizoibwa zimepatikana.Uchunguzi zaidi unaendelea" Taarifa kutoka DCI iliripoti.

 

Mhuni huyo alihojiwa kwa muda mrefu na maafisa wa polisi kabla ya kupelekwa kwenye kituo cha polisi.