Polisi wafichua jinsi kakake Eric Omondi, Fred Omondi alifariki

Fred alifariki katika ajali ya barabarani kwenye Barabara ya Outering Jumamosi asubuhi.

Muhtasari

•Polisi walisema ajali hiyo ilitokea Jumamosi asubuhi baada ya bodaboda iliyokuwa imembeba Omondi kugongwa na basi.

•Marafiki na watu mashuhuri waliotumbuiza naye walikusanyika kwenye mitandao ya kijamii kuomboleza kifo chake.

Fred Omondi
Image: HISANI

Aliyekuwa mchekeshaji wa Churchill Show Fred Omondi amefariki, polisi wamesema.

Fred, kaka wa mwanaharakati na mchekesjai maarufu  Eric Omondi alifariki katika ajali ya barabarani kwenye Barabara ya Outering Jumamosi asubuhi.

Polisi walisema ajali hiyo ilitokea Jumamosi asubuhi baada ya bodaboda iliyokuwa imembeba Omondi kugongwa na basi lililokuwa likienda mwendo kasi na kumlazimisha mwendeshaji huyo na marehemu kutua kwenye lami.

Omondi alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipokuwa akihudumiwa, afisa wa polisi alisema.

Shahidi alisema alifariki papo hapo.

Marafiki na watu mashuhuri waliotumbuiza naye walikusanyika kwenye mitandao ya kijamii kuomboleza kifo chake.

Mchekeshaji Terrence Creative alipokuwa akimuomboleza alisema alipokea simu saa kumi na mbili asubuhi Jumamosi kumjulisha kifo chake.

"Fred namshukuru Mungu kwa muda aliotupa pamoja bro, umekuwa sehemu ya kazi yangu na ukuaji katika tasnia. Ulinichukulia kama kaka na kunikaribisha wakati sikuwa na mahali pa kwenda," Terrence alisema.

"Ulinipa jukwaa na kunilipa, na kwa pamoja tulianza maonyesho ya vichekesho vya klabu. Nitathamini kila wakati tuliposhiriki jukwaa."

Mwanasiasa Millicent Omanga, alitoa rambirambi zake kwa X, akisema:

"Tasnia ya ubunifu imepoteza thamani. Fred Omondi aliangaza vyumba vyetu vya kuishi na vichekesho vyake vya uraibu. Kwamba amepoteza maisha yake katika ajali ya barabarani inahuzunisha moyo. Ninawapa pole familia yake, marafiki, na mashabiki wake. Naomb nafsi yake ipate amani kamili."

Mwanamuziki Nameless naye alimlilia.

“Hii imezidi... maisha ni tete! Pumzika vizuri Fred! Habari za kusikitisha kama hizo! Pole za dhati kwa familia!!