KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumapili

Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Muhtasari

•Baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. 

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Busia, Siaya, Bungoma, na Laikipia.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Juni 16. 

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Busia, Siaya, Bungoma, na Laikipia.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mitaa ya Donholm, Savannah, Dakar Road, Saika, na Umoja 3 zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Mumias na Ingotse katika kaunti ya Kakamega zitakosa umeme kati ya saa sita mchana na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Busia na Rwambwa katika kaunti ya Busia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa sita mchana na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Siaya, baadhi ya sehemu za maeneo ya Ugunja na Nyamninia zitakosa umeme kati ya saa sita mchana na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, Sehemu kadhaa za mji wa Bungoma katika kaunti ya Bungoma pia zitaathirika.

Mji mzima wa Nanyuki katika kaunti ya Laikipia utakosa umeme kati ya  saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.