Orodha kamilifu ya baraza la mawaziri lilolovunjwa na mawaziri kutimuliwa na rais Ruto

Rais alisema mambo ya Wizara kuanzia sasa yataratibiwa na Makatibu Wakuu hadi baraza la mawaziri litakapoteuliwa.

Muhtasari

• Mkuu wa Nchi alisema baraza jipya la mawaziri litatajwa baada ya mashauriano ya kina katika sekta zote.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto amelivunja Baraza lake la Mawaziri na kuwarudisha nyumbani mawaziri wote na mwanasheria mkuu.

Uamuzi huo hauathiri Waziri Mkuu Musalia Mudavadi na naibu rais Rigathi Gachagua.

Hii hapa ni orodha ya waliotimuliwa;

Waziri                                                     Wizara

1.Kithure Kindiki                 Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa

2.Njuguna Ndung'u           Wizara ya Hazina ya Kitaifa na Mipango 

3.Aisha Jumwa                   Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi

4.Aden Duale                         Wizara ya Ulinzi 

5.Alice Wahome                  Wizara ya Ardhi, Ujenzi wa Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji

6.Alfred Mutua,                   Wizara ya Utalii na Wanyamapori

7.Moses K. Kuria                   Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Utoaji

8.Rebecca Miano                Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda

9.Kipchumba Murkomen             Wizara ya Barabara na Uchukuzi

10.Zacharia Mwangi Njeru                          Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji 

11.Peninah Malonza,                 Jumuiya ya Afrika Mashariki, 'The ASALs & Regional Development'

12.Mithika Linturi                             Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo

13. Ezekiel Machogu                        Wizara ya Elimu 

14..Davis Chirchir                                 Wizara ya Nishati na Petroli

15.Ababu Namwamba                    Wizara ya Masuala ya Vijana na Michezo 

16.Simon Chelugui               Wizara ya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na za Kati

17.Salim Mvurya                                  Wizara ya Madini, Uchumi wa 'Bluu' na Masuala ya Bahari

18.Florence Bore                                     Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii

19.Susan Nakhumicha Wafula           Wizara ya Afya

20.Eliud Owalo                  Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali

21.Roselinda Soipan Tuya         Wizara ya mazingira na Misitu

22.Mercy Kiiru        katibu wa baraza la mwaziri 

23.Justin Muturi    Mwanasheria mkuu wa serikali