Kisa kingine cha moto charipotiwa shule ya Ortum Boys, kaunti ya West Pokot

Hiki ni kisa cha nne cha moto kuripotiwa shuleni katika kipindi cha siku 3, tangu mkasa wa moto uliowaua wanafunzi 21 katika shule ya Hillside Endarasha, kaunti ya Nyeri.

Muhtasari

• Hiki ni kisa cha nne cha moto kuripotiwa shuleni katika kipindi cha siku 3,

Picha ya nyumba inayowaka moto
Image: Hisani

Kisa kingine cha moto shuleni kimeripotiwa katika shule ya wavulana ya Ortum katika kaunti ya West Pokot.

Hiki ni kisa cha nne cha moto kuripotiwa shuleni katika kipindi cha siku 3, tangu mkasa wa moto uliowaua wanafunzi 21 katika shule ya Hillside Endarasha, kaunti ya Nyeri.

Video zinazosambaa mtandaoni zinaonyesha wanafunzi, waliovalia suruali nyeusi na sweta za kijivu, wakikimbia kutokana na moshi mzito uliokuwa ukifuka kutoka katika mabweni yao.

Katikati ya machafuko hayo, baadhi ya wanafunzi walionekana wakijaribu kuokoa magodoro na mali zao nyingine.

Moto huo ulioanza mwendo wa saa 9:00 asubuhi, uliteketeza kwa haraka bweni moja kuu na kusambaa hadi mengine na kusababisha taharuki kwa jamii ya shule hiyo.

Visa vingine vya moto shuleni vimeripotiwa tangu Ijumaa wiki jana katika shule za upili kama vile ya wavulana na Njia kaunti ya Meru, ya wasichana ya Isiolo, ya wavulana na St Peter Clever kauunti ya Makueni na ile ya Maiani katika kaunti hiyo ambazo zote zimesalia kufungwa.