KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa stima leo, Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 19.

Muhtasari

•Katika taarifa ya Jumatano jioni, KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Kajiado, Isiolo, Muranga, na Kisii.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 19. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Kajiado, Isiolo, Muranga, na Kisii.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa General Mathenge zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Thindigua katika kaunti ya Kiambu litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Namanga na Bissil katika kaunti ya Kajiado yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Isiolo, maeneo ya Maili Saba na Maili Tatu yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Olivando katika kaunti ya Murang'a litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kiabusura na Motonto katika kaunti ya Kisii pia yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.