Kanisa la kipentekosto lapinga msuada kudhibiti makanisa

Kanisa la kipentekosto lakashifu vikali bili la seneti kwa makanisa wakiitaka serikali kuchukuwa maoni ya wananchi

Muhtasari

•Bili ambayo ilitolewa kwa makanisa na dini yapata changamoto baada ya muungana wa kanisa la pentekosto kukashifu vikali bili hiyo wakiitaka serikali kuchukua maoni ya wananchi.

CROSS
Image: HISANI

Muungano wa makanisa ya kipentekosto unapinga msuada wa seneti kuhusu makanisa. 

Wakizungumzia kutoka Nakuru,kwa ufunguzi wa taasisi za kipentekosi (APVOTIK), Kasisi Ezekiel Mwendo na ambaye ndiye katibu mkuu wa muungano huo alisema kuwa msuada huo unafaa kupelekwa bungeni ili upigwe msasa.Vile vile ameitaka serikali kuchukua maoni ya wananchi.

Aliongeza kusema kuwa lazima kanisa lihusishwe ndiposa watoe maoni yao kuhusiana na swala hilo.

Msuda huo wa dini, 2024 ,inatoa mfumo mpya wa utendakazi kwa makanisa na dini zinginezo ambazo ziko na taasisi za mafunzo.Aidha,mfumo huo unatoa adhabu kali kwa taasisi za makanisa ambazo hazitakuwa zimejiandikisha akisema hiyo sio sahihi.

Kwa sasa bili hiyo tayari ishaa pitia kuangaliwa mara ya kweanza.Kwenye hiyo bili,wahudumu wa makanisa ambayo watatao sarakasi za miujiza ili kupata hela watatozwa kima cha Ksh.5 milioni au kifungo cha miaka 10.

Aidha kwenye bili hiyo ,inadokeza kuwa lazima watu takriban 25, ndiposa kiweze kuwa kwenye mwavuli wa kidini ambao unafaida kwa taarifa ya bili hiyo.

Aidha, Bishop Dr. Caleb Oruko alidokeza hatua ya bili hiyo kufikia hapo haikupitia matakwa ya umma.