Ni kuhusu 2027, Hakuna kingine, akiri Kimani Ichung'wah

Joto la kisiasa nchini limesababisha msambaratiko baina ya viongozi kutoka eneo la mlima Kenya

Muhtasari

• Ichung'wah ameendelea kukashifu naibu wa rais akidai kuwa ameonja uongozi na sasa ana njaa ya madaraka.

• Viongozi wa kutoka eneola mlima Kenya wametofautiana kuhusu kionozi wa eneo hilo pana katika vita vya kisiasa vinqavyomhusisha naibu wa rais Rigathi Gachagua

Image: HISANI

Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung'wah amekiri kuwa joto la kisiasa linaloendelea kwa sasa nchini ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kupitia mtandao wako wa X, mbunge Ichung'wah amesema kuwa matukio yanayoshuhudiwa kisiasa nchini ni  kuhusu urithi wa uongozi.

Ichungw'ah mnano tarehe 20 Septemba alibandika video ya naibu wa Rais Rigathi Gachagua akisema kuwa kiongozi huyo analenga kuleta ukosefu wa utulivu wa kisiasa akipigia mfano wa tarehe 25 Juni, ambapo waandamaji walifaulu kuingia bungeni.

Kulingana na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa ni kuwa, naibu wa rais anajaribu kuwahadaa Wakenya serikali ya Kenya pamoja na Rais.

"Hivi ndivyo uchochezi wote katika mkoa mmoja unahusu," aliongeza kuandika Ichung'wah.

Kwa muda sasa, kumeonekana kuwepo mgawanyiko katika uongozi wa UDA haswa baina ya rais na naibu wanasiasa kutoka mkoa wa kati wakionekana kutofautiana na naibu wa rais wakimshutumu kufanya siasa la kugawanya Wakenya kimaeneo.

Aidha, Jumamosi 21, mbunge Ichung'wah pia aliweka ujumbe katika ukurasa wake wa X akisema kuwa matukio yote ya kisiasa yanayoendelea nchini yanahusu uchaguzi wa mwaka 2027.

Ichung'wah aliandika kuwa ukosoaji mkali wa kikabila, sauti za chini za kikabila, vitisho vya kukosekana kwa utulivu zimeshamiri.

Hata hivyo, katika ujumbe huo ambao umeonekana kumlenga naibu rais, Kimani Ichung'wah amesema kuwa, "Mwanaume ameonja utawala, sasa ana njaa ya madaraka na amepofushwa na ulafi."