Jenerali Muhoozi akaidi marufuku ya rais wa Uganda

Muhtasari
  • Muhoozi kupitia kwenye mtandao huo huo amejibu madai hayo na kusema kwamba hamna mtu yeyote atakaye mkomesha kufanya jambo lolote
KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Siku moja baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameweka wazi kwamba atamshrutisha jenerali mkuu wa majeshi ya Uganda, Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni mwanawe kukoma kutumia mtandao wa Twitter,Muhoozi amejibu madai hayo.

Muhoozi kupitia kwenye mtandao huo huo amejibu madai hayo na kusema kwamba hamna mtu yeyote atakaye mkomesha kufanya jambo lolote.

Jenerali wa jeshi mwenye utata ambaye hivi majuzi alizua dhoruba mtandaoni baada ya kutuma ujumbe Twitter kuhusu mpango unaodaiwa kuivamia Kenya alienda kwenye mtandao wa kijamii Jumanne usiku kusisitiza kuwa yeye ni mwanasiasa. mtu mzima ambaye hawezi kupigwa marufuku na chochote.

“Nasikia mwanahabari fulani kutoka Kenya alimwomba babangu anipige marufuku kutoka kwa Twitter? Je, huo ni utani fulani?? Mimi ni mtu mzima na HAKUNA MTU atakayenipiga marufuku kwa lolote!” alisema.

Museveni ambaye alikuwa na mahojiano ya kipekee na mwanahabari wa Kenya Sophia Wanuna alisema kwamba mtandao wa Twitter si mbaya bali kinachozingatiwa ni kile ambacho mtu anapakia kule.

“Unatazamia kumwambia Muhoozi kutoka Twitter pengine?” Wanuna alimuuliza Museveni.

“Jenerali Muhoozi ataondoka Twitter. Tumekuwa na mjadala huu, unajua Twitter sasa hivi ni njia ya kisasa ya kuwasiliana, na yeye ameungana na vijana wenzake ambao anafanya mambo nao, lakini suala ni kuhusu ni kile unachotweet,” Museveni alijibu.