Mtoto wa Chebukati amsherehekea kwa kutuzwa heshima ya kiraia ya EGH na rais Ruto

Baada ya miaka 6 ya uongozi wa tume ya uchaguzi ya Kenya, yake ni hadithi ya "damu, taabu, machozi, na jasho - Emmanuel alisema.

Muhtasari

• Chebukati alitunukiwa heshima hiyo na rais Ruto baada ya sherehe za Jamhuri.

• Kwa mara kadhaa, Ruto amekuwa akimtaja Chebukati kama shujaa aliyehakikisha uchaguzi ni wa haki na uwazi.

Chebukati alitunukiwa heshima ya kiraia ya EGH na rais William Ruto.
Chebukati alitunukiwa heshima ya kiraia ya EGH na rais William Ruto.
Image: Twitter

Jumatatu baada ya kukamilika kwa sherehe za Jamhuri ugani Nyayo, rais Ruto aliwatuza watu mbalimbali tuzo za kuonesha ushujaa wao katika taifa la Kenya.

Mmoja aliyebahatika kuwa miongoni mwa wale waliotambulika kwa tuzo za kishujaa ni mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, Wafula Chebukati.

Chebukati alivishwa  taji la ‘Elder of Order of Golden Heart’ EGH na rais Kenyatta kwa juhudi zake za kuendesha uchaguzi ambao rais Ruto kwa mara kadhaa amekuwa akiutaja kama wa haki na uwazi licha ya pingamizi kali kutoka kwa mrengo wa wapinzani.

Mtoto wa Chebukati, Emmanuel Chebukati hakustia kumsherehekea babake kwa taji hilo kubwa ambalo daima litakuwa linaambatanishwa na jina lake rasmi.

Kupitia Twitter, Emmanuel alimsifia babake na kusema kuwa kwa miaka 6 ambayo amekuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo muhimu katika uongozi wan chi, amekuwa mstahimilifu wa kupambana na kutoshwa jasho ili kuhakikisha nchi inabaki katika njia kuu pasi na machafuko.

“Leo @WChebukati alitunukiwa Mzee wa Agizo la Moyo wa Dhahabu (EGH), heshima ya juu zaidi ya kiraia nchini Kenya. Baada ya miaka 6 ya uongozi wa tume ya uchaguzi ya Kenya, yake ni hadithi ya "damu, taabu, machozi, na jasho" kufanya jambo sahihi kwa gharama yoyote. Unastahili, baba!” Emmanuel alimvisha koja la maua babake.