Mashtaka ya kumuondoa madarakani Gavana Mwangaza hayana maana-Omanga

Omanga alisema mashtaka dhidi ya Mwangaza hayana nguvu inayoweza kumfungulia mashtaka.

Muhtasari
  • Kamati hiyo itafanya vikao kwa siku mbili kabla ya kurejea kuandika uamuzi wake kulingana na ushahidi uliotolewa
Seneta mteule Millicent Omanga
Seneta mteule Millicent Omanga
Image: TWITTER//MILLICENTOMANGA

Aliyekuwa seneta mteule Millicent Omanga amekazania kesi inayoendelea ya kushtakiwa kwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza.

Omanga alisema mashtaka dhidi ya Mwangaza hayana nguvu inayoweza kumfungulia mashtaka.

"Naona mashtaka ya kumuondoa madarakani Gavana Kawira Mwangaza hayana maana - hayana nguvu na uimara," aliandika kwenye ukurasa wake twitter siku ya Jumatano.

Msemaji wa Azimio Makau Mutua pia alikagua suala hilo akisema hakufurahishwa na jinsi Mwangaza ameendesha shughuli za Meru tangu kuchaguliwa kwake lakini haoni ukiukaji wowote katika uongozi wake kwamba itakuwa ni hatia.

"Sijafurahishwa na jinsi Gavana Kawira Mwangaza ameendesha Kaunti ya Meru kufikia sasa, lakini hajatenda kosa hata moja," alisema kwenye taarifa kwenye mtandao wa kijamii.

Mutua alisema kuwaondoa ni shughuli nzito na lazima ishughulikiwe kwa uangalifu mkubwa.

Kamati hiyo itafanya vikao kwa siku mbili kabla ya kurejea kuandika uamuzi wake kulingana na ushahidi uliotolewa.