Mchungaji afunga kanisa baada ya kushinda shilingi milioni 3.5 kwa ku'bet

Lazima nikiri nilifungua kanisa hili kutokana na tamaa lakini si upako. Niliona jinsi wachungaji kadhaa wanavyopata pesa kwa kuwa na umati mkubwa kanisani,"

Muhtasari

• Baadae alisema kuwa alikosa furaha alipoanza kupata ndoto za ajabu.

• Wakati mmoja aliamua kuwekeza katika mchezo wa kamari na bahati ikasimama upande wake, hivyo kughairi nia yake kuendelea kama mchungaji.

Pesa za Kenya
Pesa za Kenya
Image: HISANI

Mchungaji katika kanisa moja nchini Uganda amewaacha waumini wa kanisa lake kwa kulifunga kanisa hilo baada ya kujishindia Shilingi Milioni 100 za Uganda ambazo ni kiasi sawa na milioni 3.5 pesa za Kenya kutokana na kamari ya michezo.

Akielezea sababu zake, mchungaji huyo aliyejawa na furaha alifichua kuwa bahati nasibu hiyo ilitumwa na Mungu na njia ya haraka ya kumtoa kwenye umaskini kwani amekuwa akiteseka.

Aidha alifichua kuwa alifungua kanisa kama chanzo cha mapato na sio kupitia upako, Jarida moja liiripoti.

“Lazima nikiri nilifungua kanisa hili kutokana na tamaa lakini si upako. Niliona jinsi wachungaji kadhaa wanavyopata pesa kwa kuwa na umati mkubwa na kutoa unabii wa uwongo ili kuvutia zaidi,” alifunguka.

Alisema kuwa kuendesha kanisa bila wito imekuwa ngumu sana na kusababisha kukosa usingizi usiku. Akiwa amelemewa na hatia, pasta aliamua kuifunga na kutafuta njia nyingine za kupata pesa.

“Kadiri muda ulivyosonga, niligundua kuwa hii haikuwa sawa; Nilianza kukosa usingizi na siku zote ningekuwa na ndoto za ajabu. Kabla sijafungua kanisa hili, kila kitu kilikuwa cha kawaida upande wangu. Hata bila pesa, sikuwa na ndoto yoyote ya ajabu. Kwa hiyo niliamua kukomesha hili na kutafuta njia nyingine za kupata pesa,” Alisema.

Kasisi huyo alisema kwamba alijaribu bahati yake kwa kucheza kamari, na kuweka kiasi kikubwa cha Ush1 milioni kama hisa.

“Ilinibidi kulipia michezo hii na cha kushangaza ilinichukua takriban mwezi mmoja kuipokea. Waliniambia walikuwa na maswala na mfumo wao na mchakato wa kupata michezo huchukua muda. Nilikaribia kukata tamaa na kuwaita matapeli lakini waliwasiliana nami kwa maelezo na wow! Nilikwenda kikamilifu na kupata, " Alinukuliwa na blogu moja ya Uganda.

Hapo ndipo alipoacha kwenda kanisani alipogundua kwamba alipata pesa nyingi zaidi katika kucheza kamari kuliko alivyokuwa amewahi kulea kuendesha kanisa au maisha yake yote.