Video: Genge la majambazi wenye bunduki wavamia studio ya redio na kutekeleza wizi

Katika video hiyo, wezi hao watatu waliokuwa wamejifunika nyuso kwa hancifu walikuwa na bunduki na kutimba studioni wakiwaamrisha watangazaji kuzima kila kitu.

Muhtasari

• Kipindi wanaingia studioni, watangazaji walikuwa wanaendelea na kipindi moja kwa mpoja ambapo pia walikuwa 'live' kwenye Facebok.

Genge la wezi wenye bunduki wavamia kituo cha redio na kutekeleza wizi
Genge la wezi wenye bunduki wavamia kituo cha redio na kutekeleza wizi
Image: BBC NEWS

Majambazi waliokuwa na bunduki walivamia kituo cha redio cha Injili chenye makao yake mjini Nakuru mnamo Alhamisi, Mei 11, huku watangazaji wake wa jioni wakiwa hewani.

Katika video iliyoonekana na Radio Jambo na ambayo imeenezwa mitandaoni, watangazaji wa redio ya Mwinjoyo FM walikuwa na wakati mzuri kuwaburudisha wasikilizaji wao wakati genge la wanaume watatu waliovalia kofia walipoingia.

“Zima hio kitu. Zima haraka!” aliamuru mmoja wa majambazi hao wakati wenzake wakiendelea na kupora studio.

Kisha watangazaji waliamriwa kulala chini wanaume hao wakizunguka studio yao.

“Ni nini unafanya wewe?” aliuliza mmoja wa majambazi hao kabla ya kumpiga teke mtangazaji mmoja ambaye tayari alikuwa amelala chini.

Video hiyo ya kushangaza ya dakika tatu ilionyesha mmoja wa wanaume hao akiwa na bunduki huku mwingine akitembea na panga.

“Nani ako huko juu?” genge liliwauliza watangazaji mara kwa mara.

Wakati wote wa majaribu hayo, waliendelea kukagua mlango wa kuingilia ikiwa kuna mtu anayeingia ndani yao.

Baada ya dakika chache ndani ya studio, waligundua kuwa shughuli yao mbaya inaweza kuwa imenaswa kwenye CCTV.

“CCTV iko wapi? CCTV iko wapi?" waliuliza.

Waathiriwa walitii kwa busara na kuwaonyesha mahali ilipo CCTV.

"Na uko kwenye Facebook Live?" waliuliza.

Wakati huo, walichukua simu iliyokuwa ikirekodi wizi huo na kuizima.

Washiriki wa genge hilo walikuwa na vinyago kuficha utambulisho wao. Waliondoa simu na vifaa vingine vya studio.

Hii hapa video ya tukio hilo la kubementa akili: