KIZUNGU CHAMPIGA CHENGA DP

Gachagua amtaka Wetang'ula kulegeza Kizungu chake akitoa hutuba

Naomba upunguze Kizungu ili niweze kuelewa kile ambacho unasema

Muhtasari

•Tafadhali bwana Speaker, iwapo utanialika kuzungumza tena naomba uwe mzingatifu kimpango, uweze kupunguzu Kizunguzu ili niweze kuyapa uyasemayo.

•Anapaswa kuniheshimu maana pia kwa miaka 35 sasa bibi yangu wa Alliance Girls bado tuko pamoja.

NAIBU RAIS RIGATHI GAHAGUA
Image: HISANI

Naibu Rais Rigathi Gachagua amemsihi Spika wa Bunge la Kitaifa  Moses Wetangula kulegeza Kizungu chake ili kieleweke. 

Gachagua amesema hili katika hafla ya ibada ya maombi ya kitaifa iliyoongozwa na wabunge jijini Nairobi siku ya Jumatano.

“Tafadhali bwana Speaker, iwapo utanialika kuzungumza tena katika hafla nyingine ile, naomba uwe mzingatifu kimpango, uweze kupunguza Kizunguzu ili niweze kuyapata uyasemayo.” Gachagua alisema.

Alisema hili alipokuwa akieleze kuwa, hakupata nafasi ya kusomea katika shule tajika ikilinganishwa na mwenzake mbunge Kimani Ichungwa au pia baadhi ya wakuu serikalini.“ Kimani Ichungwa hujaribu kututania mimi na Rais licha ya kuwa wakubwa wake kwa sababu alisomea shule ya upili ya Alliance High.” Alieleza. 

Gachagua alijisifu kuwa pia naye anafaa kutambuliwa maana alienda Alliance Girls akamchanganya binti wa mtu na ambaye kwa sasa ndiye mke wake. “Nilienda Alliance Girls, nikamchanganya msichana wa mtu, na sasa ni bibi yangu. Wao walienda uko na hawakupata bibi, kwa hivyo nani mkubwa?” Aliuliza.

Wakati wa hafla hiyo ya maombi Rais William Ruto ametangaza kuwa kila mwezi wa Mei  kutakuwa na maombi ya kitaifa ili kuliombea taifa ambalo limekumbwa na mambo mengi.