HALI YA UCHUMI

Mswada wa fedha, Azimio kutoa mustakabali wake Jumanne wiki ijayo

Tunawaalika Wakenya Jumanne wiki ijayo katika Uwanja wa Kamukunji, tushauriane juu ya mstakabali wa taifa

Muhtasari

•Iwapo sheria hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi wa Julai, gaharama ya maisha inatarajiwa kupanda marudufu.

• Karua alisema kuwa wataeleza wakenya hatua watakayochukuwa baada ya msuda huo tata kupitishwa bungeni. 

Image: Martha Karua// Twitter

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, umeahidi Wakenya kutoa mstakabali wa taifa siku ya Jumanne wiki ijayo, kuhusu mswada tata wa fedha wa mwaka 2023 uliopitishwa bungeni siku chache zilizopita.

Akiwahutubia wanahabari  siku ya Alhamisi kiongozi wa chama cha NARC Kenya Martha Karua, akiandamana na baadhi ya viongozi wa muungano huo, alisema kuwa wataeleza wakenya hatua watakayochukuwa baada ya msuda huo tata kupitishwa bungeni. 

Karua alisema mswada huo unajumuisha vipengele vinavyodhalilisha wananchi. Alitaja ushuru wa 16% kwa mafuta ya petroli na 1.5 ya ushuru wa nyumba kama moja wapo ya vipengele vitakavyofanya maisha ya wakenya kuwa magumu hata zaidi na kuongeza gharama ya maisha. 

"Kwa wabunge ambao kwa kujua waliunga mkono mswada uliokataliwa kwa wingi na Wakenya, tunawaambia kwamba  kifungo chenu kiko wazi. Siku yenu ya kuhesabiwa itafika,” Karua alisema.

Karua aliendelea  kusema kuwa, wamewaalika Wakenya kwa mashauriano  siku ya Jumanne katika uwanja wa Kamukunji, saa nne za asbuhi ambapo watawaambia hatua itakayofuata.

“Tumeamua kuwaalika Wakenya kwa mashauriano katika uwanja wa Kamukunji Jumanne ijayo tarehe 27 Juni saa 10 asubuhi, ambapo hatua inayofuata itaamuliwa. Tunaamini sauti ya watu itafanikiwa.Aliendelea.

Iwapo sheria hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi wa Julai, gaharama ya maisha inatarajiwa kupanda marudufu, ambapo mshahara wa Wakenya unatarajiwa kupungua kutoka na makato mbali mbali yaliopendekezwa. 

Haya yanajiri wakati Rais William Ruto amesema kuwa, hakumhonga  mbunge yeyote katika kuupitisha mswada tata ambapo alikanusha madai kuwa alitoa shilingi milioni moja kwa kila mbunge aliyeupitisha mswada huo.