USHURU KATIKA NCHI

Wafuasi wa Azimio la Umoja wamsubiri Raila Odinga Kamukunji

Walisikika wakiimba Zakayo shuka, huku wametia sufuria changarawe.

Muhtasari

• Raila Odinga, anatarajiwa wakati wowote kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, kutoka Dubai ili aweze kuwapa wafuasi wake mustakabali juu ya sheria iliyopitishwa jana.

Wanaazimio katika uwanja wa Kamukunji, Nairobi
Wanaazimio katika uwanja wa Kamukunji, Nairobi
Image: Picha na ENOS TECHE

Wafuasi wa muungano wa upinzani wamemsubiri kinara wao Raila Odinga kujiunga nao ili kuweza kushauriana ni yapi yatakayofuata kuhusiana na sheria ya ushuru katika fedha.

Image: ENOS TECHE

Raila Odinga, anatarajiwa wakati wowote kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, kutoka Dubai ili aweze kuwapa wafuasi wake mustakabali juu ya sheria iliyopitishwa jana.

Image: ENOS TECHE

Kulingana na  raia, wamehisi kuwa watakuwa katika hali ya hatari kuanzia mwezi ujao wa Julai, na hivyo kumhitaji mkuu huyo wa Azimio awape maelezo zaidi, wakitarajia kutangazwa kwa maandamano ya kitaifa.