Chizi amshambulia padri wa Katoliki kanisani na kumuua kwa kumpiga kitu kizito kichwani

Mtu huyo, alikuwa akilazimisha kuingia kanisani kusali tangu usiku wa kuamkia Alhamisi lakini akazuiliwa na walinzi, asubuhi Padri akawataka kumruhusu kuingia kanisani kwa lengo la kusali.

Muhtasari

• Mtu huyo aliingia kanisani kwa fujo akionesha nia ya kwenda kusali kabla ya kumshambulia papa paroko huyo mkongwe.

• Mtu huyo naye hakusalimika kutoka mikononi mwa watu weney ghadhabu waliowahi kanisani hapo kabla hajatoroka kutoka eneo la mkasa.

Chizi amuuwa padri kanisani.
KANISANI Chizi amuuwa padri kanisani.
Image: Screengrab

Kanisa katoliki katika nchi jirani ya Tanzania jimbo la Arusha linaomboleza.

Hii ni baada ya taarifa kuzuka kwamba padre mkuu wa kanisa katoliki katika parokia ya Karatu mkoani humo aliyetambulika kwa jina Pamphili Nada kuawa kwa kushambuliwa na mtu aliyeingia kanisani kwa lengo la kusali.

Kwa mujibu wa jarida la Mwananchi, Pamphili aliangamia kifo baada ya kupigwa na kifaa kizito kichwani na mtu anayesadikika kuwa na matatizo ya afya ya akili.

Mtu huyo aliingia kanisani kwa fujo akionesha nia ya kwenda kusali kabla ya kumshambulia papa paroko huyo mkongwe.

Mtu huyo naye hakusalimika kutoka mikononi mwa watu weney ghadhabu waliowahi kanisani hapo kabla hajatoroka kutoka eneo la mkasa.

Jarida hilo lilimtambua chizi huyo kama Romani Leonard mwenye umri wa miaka 30, ambaye pia alishambuliwa na umati hadi kufa.

"Padri alifariki wakati anapelekwa hospitali na mtuhumiwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo," kamanda wa polisi mkoani Arusha, Justine Masejo aliambia jarida hilo.

Wakizungumza na Mwananchi Digital baadhi ya wakazi wa Karatu walisema mtu huyo, alikuwa akilazimisha kuingia kanisani kusali tangu usiku wa kuamkia Alhamisi, hata hivyo hakufankiwa baada ya walinzi kumzuia.

Mmoja wa wakazi hao alisema hata hivyo ilipofika alfajiri mtu huyo aliendelea kupiga kelele kutaka kuingia kusali na ndipo Padri Nada alitoka nje na kumwambia mlinzi amfungulie mlango.

Kutokana na tukio hilo kengere ya kanisa ilipigwa na wananchi kukusanyika na baada ya kupata taarifa hizo walianza kumpiga mtu huyo na kusababisha kifo chake pia.