Mrembo atoa mimba na kuweka kijusi mfukoni kisha kumkabidhi mhusika kwenda kukizika

Msichana huyo alikuwa anaishi na mama wa kambo aliyemshurutisha kutoa mimba ili kuolewa na kijana mwingine aliyekuwa amemtafutia.

Muhtasari

• Watu wa eneo hilo walikilaani kitendo hicho huku lawama zikielekezwa kwa mama wa kambo aliyesemekana kumshrutisha binti huyo kuavya mimba.

Jamaa azunguka na kijusi
Jamaa azunguka na kijusi
Image: Screengrab

Kioja kilishuhudiwa baada ya kijana wa umri wa makamo kupatikana mitaani akiwa na kijusi kwenye mfuko akizunguka nacho mitaani kwa lengo la kutafuta pa kukitupa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, mama wa kambo alimshauri binti aliyekuwa anaishi naye kuavya mimba na kumpelekea mwanamume aliyehusika kichanga hicho ndani ya mfuko wa kufanyia ununuzi ili kwenda kukizika anakojua mwenyewe.

Tukio hilo liliripotiwa kufanyika mkoani Arusha katika taifa jirani la Tanzania.

Mashuhuda wa tukio hilo waliambia vyombo vya habari nchini humo kwamba kijana huyo aliletewa kijusi hicho ndani ya mfuko wa kununulia bidhaa za kula na mrembo huyo baada ya mama wa kambo kushurutisha kutoa ujauzito huo.

Mama huyo alitaka binti huyo atoe ujauzito ili aolewe na mwanamume mwingine.

“Huyu mama alimtoa mimba kilazima na huyu alikuwa amekaribia kufa ndio mama wa kambo alimpigia bwanake simu na wakapotezea. Yule msichana si alikwenda kutupa kile kijusi, sasa badala ya kutupa akampelekea baba mhusika. Huyu ndio akakuja na ule mzigo akituomba ushauri afanyeje, mimi ndio nikamshauri twende kituoni,” mmoja wa mashuhuda alisema.

Watu wa eneo hilo walikilaani kitendo hicho huku lawama zikielekezwa kwa mama wa kambo aliyesemekana kumshrutisha binti huyo kuavya mimba.

Baadhi walimlaumu binti huyo kwa kupokea ushauri wa mama wa kambo kama kipofu bila kuchanganua maamuzi yake, ikisemekana kwamab alikuwa anataka kuishi na mwanamume mwingine bila mzigo wa mtu mwingine.