Pia wewe utakufa siku moja-Mackenzie amwambia hakimu

Alieleza kuwa kila mtu wakiwemo viongozi hao hatimaye watafariki dunia, akiiomba mahakama kumsaidia.

Muhtasari
  • Mhubiri huyo mwenye utata aliomba mahakama itoe picha kutoka kwa CCTV ili kumuondolea mashtaka ya kufufua huduma yake iliyoharamishwa.
Mchungaji Paul Mackenzie

Mackenzie na washtakiwa wenzake walifikishwa mbele ya Mahakama ya Sheria ya Shanzu mnamo Ijumaa, Agosti 4, kusikizwa kwa maombi ya upande wa mashtaka ya kuwazuilia kwa siku 47 zaidi.

Mhubiri huyo mwenye utata aliomba mahakama itoe picha kutoka kwa CCTV ili kumuondolea mashtaka ya kufufua huduma yake iliyoharamishwa.

Alieleza kwamba alipata kanisa lililoanzishwa huko Shimo La Tewa muda mrefu kabla ya kuzuiliwa, akihoji kwa nini wenye mamlaka hawakulisimamisha.

"Naomba korti iitishe CCTV footage iko kwa hiyo block ambayo tumekuwa ilete picha ili ionekane ni wapi nimeconduct a church service na zaidi ya hiyo kanisa anayosema isiwe gerezani kabla sijafiak shimo la tewa nimeingia nikakuta kanisa tayari linaendelea. Mbona hilo hajasimamisha," alisema.

Mackenzie aliyekasirika alithubutu maafisa wamuue na kutupa mabaki yake katika Mto Yala akimaanisha miili ambayo haikudaiwa kupatikana mtoni.

Alieleza kuwa kila mtu wakiwemo viongozi hao hatimaye watafariki dunia, akiiomba mahakama kumsaidia.

Katika video inayosambaa mitandaoni Mackenzie alionekana kumkashifu hakimu wa mahakama,kwa kunyimwa nafasi ya kuota jua.

"Mimi nina kichwa. Mkiona hata mmechoka na mimi na hawa wenzangu, tuko tayari mtupeleke River Yala. Hatuna shida na hiyo. Kwa sababu mimi nitakufa na wewe pia siku moja utakufa, hakuna mahali utaenda hivyo. Kwa hii korti inisaidie nimefungiwa katika giza na nina kufa kwa ajili ya baridi naomba tu nafasi angalu ya kuota jua," aliongeza.