Aliyekuwa mwanahabari wa michezo NTV Sean Cardovilis azirai na kufariki nyumbani

Mpaka kifo chake, Sean Cardovillis alikuwa anafanya kazi Capital FM na ilisemekana alikuwa alipaswa kuwa kazini Jumamosi alasiri. Pia aliratibiwa kufanya mahojiano Faith Kipyegon.

Muhtasari

• Haijabainika ikiwa alikuwa anaondoka kwenda kazini au alifariki Ijumaa usiku, polisi walisema.

• Mpaka kifo chake, Sean Cardovilis alikuwa anafnaya kazi katika kituo cha redio cha Capital FM humu nchini.

Sean Cardovillis
Image: Facebook

Mwanahabari wa muda mrefu wa habari za michezo humu nchini Sean Cardovilis ameripotiwa kufariki nyumbani kwake baada ya kuzirai.

Alipatikana amekufa nje ya nyumba yake huko Westlands, Nairobi

Polisi walisema mwili wa Cardovillis ulipatikana Jumamosi, Septemba 9 asubuhi nje ya nyumba yake kando ya Barabara ya Rhapta, Westlands alikokuwa akiishi peke yake.

Haijabainika ikiwa alikuwa anaondoka kwenda kazini au alifariki Ijumaa usiku, polisi walisema.

Mpaka kifo chake, Sean Cardovilis alikuwa anafnaya kazi katika kituo cha redio cha Capital FM humu nchini.

 Sean Cardovilis amekuwa akiugua mara kwa mara na itakumbukwa mwaka mmoja uliopita RadioJambo.co.ke tuliripoti kwamba alikuwa ameomba msaada wa pesa za kulipia bili ya matibabu yake ambayo ilikuwa imekwea.

Cardovilis ambaye alikuwa mwanahabari wa michezo katika runinga ya NTV aliondoka huko baada ya janga la Corona kubisha hodi nchini, jambo lililosababishia mashirika mengi na makampuni kupunguza wafanyakazi wake.

Cardovilis ambaye ana uzoefu wa kazi kwa Zaidi ya miaka 20 alifutwa kazi Pamoja na wenzake kama vile Ken Mijungu na Debarl Inea baada ya janga la Corona kulemaza shughuli nyingi za shirika la Nation.

Wakati huo akihitaji msaada, bango la kuomba msaada huo lilienezwa mitandaoni na wanahabari wa michezo akiwemo Carol Radul ambao waliwaomba Wakenya na mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi ili kusimama na mmoja wao katika matibabu.

Wafanyikazi katika kituo hicho walisema alipaswa kuwa kazini Jumamosi alasiri.

 

Alipangiwa kufanya mahojiano na bingwa kadhaa wa dunia na Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya dunia mara tatu Faith Kipyegon.

 

Alikuwa na shauku ya motocross. Mnamo Juni 2023 alirejea Capital FM baada ya miaka 18.