Mwanahabari Sean Cardovillis aomba msaada wa matibabu

Muhtasari

• Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya NTV Sean Cardovilis amahitaji msaada wa wahisani wema ili kulipia ada ya matibabu ambayo imekwea mara dufu.

Sean Cardovillis
Image: Facebook

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya NTV Sean Cardovilis amahitaji msaada wa wahisani wema ili kulipia ada ya matibabu ambayo imekwea mara dufu.

Cardovilis ambaye alikuwa mwanahabari wa michezo katika runinga hiyo aliachishwa kazi baada ya janga la Corona kubisha hodi nchini, jambo lililosababishia mashirika mengi na makampuni kupunguza wafanyakazi wake.

Cardovilis ambaye ana uzoefu wa kazi kwa Zaidi ya miaka 20 alifutwa kazi Pamoja na wenzake kama vile Ken Mijungu na Debarl Inea baada ya janga la Corona kulemaza shughuli nyingi za shirika la Nation.

Katika bango ambalo limesambazwa mitandaoni ni wanahabari na watangazaji mbali mbali, Cardovilis anahitaji msaada ili kulipia gharama ya matibabu ambayo imepiku uwezo wake na anahitaji kusaidia.

Carol Radull
Image: Facebook

“Sean amelazwa sasa kwa muda. Maumivu ya kifua aliyokuwa akiyapata kwa muda yaligeuka na kuwa nimonia na pafu lake moja likafeli. Pia alikuwa na matatizo ya moyo wake. Anazidi kupata matibabu ya kitaalamu na anaendelea vizuri lakini anahitaji ufuatiliaji na uangalizi wa karibu Zaidi,” maandiko katika bango hilo yalisoma.