'Mwanamke mzee zaidi duniani' anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 117

Dadake mwenye umri wa miaka 107 ambaye pia alikuwepo kwenye sherehe hiyo alipoulizwa siri ya kuishi maisha marefu ni gani, alijibu: Lazima ule Maharage, mahindi, mihogo, viazi.'

Muhtasari

• 'Vizazi vitano vilivyopita familia yangu ilikuwa utumwani. Walinusurika kila kitu kutoka karne iliyopita, na walishinda COVID," alielezea.

Cicera Maria dos Santos
Cicera Maria dos Santos
Image: Hisani

Mwanamke anayetajwa kuwa mkongwe Zaidi duniani amesherehekea siku yake ya kuzaliwa baada ya kufikisha miaka 117.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari kutoka Brazili, Cicera Maria dos Santos aliyezaliwa mwaka 1906 amekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa muda sasa kama mtu mkongwe Zaidi ambaye anayeishi licha ya kwamba mwezi kamili aliozaliwa haujaweza kubainika.

Ikiwa tarehe yake ya kuzaliwa itathibitishwa, itamfanya kuwa na umri wa mwaka mmoja zaidi ya mmiliki wa sasa wa Rekodi ya Dunia ya Guiness Maria Branyas Morera, 116, kutoka Uhispania.

Cicera alisherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na dadake Josefa Maria de Conceicao, 107, mnamo Septemba 23 akiwa amezungukwa na familia na marafiki.

Bash ilijumuisha keki ya rangi, vitafunio na shangwe za wageni wote, NewsFlash waliripoti.

Akina dada hao waliviambia vyombo vya habari kuwa siri ya kuishi maisha marefu ni kumwamini Mungu na kula chakula kinachofaa.

Cicera alisema: 'Amani ya Bwana iwe pamoja nasi. Nani awezaye kufanya zaidi ya Mungu? Kila kitu ni Mungu.'

Na dada yake akaongeza: 'Lazima ule Maharage, mahindi, mihogo, viazi.'

Cicera aliishi mashambani mwa Brazil kwa muda mrefu wa maisha yake.

Mjukuu wa Josefa, Ruan, alisema dada huyo mzee 'alitoka kwa watu ambao walikuwa watumwa'.

'Vizazi vitano vilivyopita familia yangu ilikuwa utumwani. Walinusurika kila kitu kutoka karne iliyopita, na walishinda COVID," alielezea.

'Furaha kuu zaidi ulimwenguni ni kuwa nao hapa leo.'

Utumwa ulifanywa nchini Brazili kuanzia katikati ya karne ya 16 hadi kukomeshwa kwake katika miaka ya 1860.

Haijulikani ikiwa Cicera au familia yake inapanga kuwasiliana na Guinness World Records ili kumfanya rasmi kuwa 'mwanamke mzee zaidi duniani'.