Video mzee akimpeleka mkewe mgonjwa hospitalini kwa baiskeli yavutia hisia

Mtumizi mmoja wa mtandao wa TikTok alijibu kaitka klipu hiyo na kusema kwamba wanandoa hao wanatoka Kaptembwa Nakuru na siku zote ajuza huyo huwa mgonjwa.

Muhtasari

• Video hiyo imepata watumiaji wengi wa TikTok wakimpongeza mzee huyo na mkewe kwa kuonyesha upendo wa kweli.

Wanandoa wakiendeshana kwa baiskeli
Wanandoa wakiendeshana kwa baiskeli
Image: TikTok

Wanamtandao wamekuwa wakitoa maoni na dhana tofauti kuhusu video ambayo imeenea kwenye mtandao wa TikTok ikimuonesha mzee mkongwe akimuendesha mkewe mkongwe pia kwenye baiskeli.

Video hiyo ilipakiwa kwenye mtandao huo na mtumizi mmoja kwa jina Miss Moraaz na kueleza jinsi alivutiwa na kitendo cha wanandoa hao wa muda mrefu kudekezana kwenye baiskeli.

Kwa mujibu wa mchapishaji huyo, alikuwa akiendesha gari lake kuingia mjini alipowaona wakiwa na baiskeli yao na mke alionekana kulemewa kiasi kwamba alihisi ndio sababu ya mumewe kumtaka kuketi kwenye kiti cha mizigo kwenye baiskeli huku yeye akiikokote baiskeli kando ya barabara kwa mwendo wa aste.

“Jamani leo nikiwa naendesha gari kuelekea mjini, niliona wanandoa hawa wazee na iliyeyusha moyo wangu. Kulikuwa na joto sana na niliweka dau kwamba mama mzee hakuweza kustahimili joto na mume aliamua kumbeba kwenye baiskeli. Ikiwa hatuzeeki hivi basi sitaki. Na ndio wamegundua hakuna kitu kinachoweza kununua furaha hata pesa yenyewe. Upendo wa kweli hushinda kila kitu na kwa hakika unaweza kuhamisha hata milima hiyo,” alisema.

Lakini kwa upande wa maoni, watu ambao wanaonekana kuwafahamu wanandoa hao kwa ukaribu waliibua dhana nyingine tofauti – na ya kutia huruma kweli kweli.

Mmoja kwa jina Blessed alitoa mtazamo tofauti ambao ulibadilisha dhana nzima, akionekana kuwa anawafahamu wanandoa hao kwa ukaribu.

Blessed alisema kwamba mzee huyo si kwamba alikuwa anajivinjari na mkewe kwa barabara bali alikuwa anakokote baiskeli kumpeleka mkewe hospitali, akisema kwamba ajuza huyo mara nyingi huwa mgonjwa.

Blessed pia alibainisha kuwa wanandoa hao ni kutoka Kaptembwa, kaunti ya Nakuru.

“Wanatoka Nakuru Kaptembwa I bet alikuwa anampeleka mkewe katika hospitali ya Nakuru level five 😌 mke anaumwa siku zote.”

Video hiyo imepata watumiaji wengi wa TikTok wakimpongeza mzee huyo na mkewe kwa kuonyesha upendo wa kweli.