Wakenya wafurika mitandaoni kumtakia Raila Odinga heri njema akifikisha miaka 79

Wengine walimsherehekea kama shujaa wa ukombozi wa uhuru wa pili miaka ya 90 huku wengine wakimtaka kiongozi huyo wa muda mrefu akiwa upinzani kama mtetezi wa wanyonge.

Muhtasari

• “Heri ya Siku ya Kuzaliwa Rt Mheshimiwa Raila Odinga, Baba wa Taifa-Rais wa Watu. Angalia 79 imara hata baada ya miaka mingi ya kuzuiliwa na Moi,” Makau Wa Muli.

Raila Odinga
Raila Odinga
Image: X

Wakenya wa matabaka mbalimbali Jumapili walifurika kwenye mitandao ya kijamii kumtakia kiongozi wa upinzanii Raila Odinga heri njema za siku yake ya kuzaliwa.

Raila Odinga anaadhimisha miaka 79 duniani.

Kwenye mtandao wa X, Wakenya wengi na baadhi ya wanasiasa walimuandikia Odinga jumbe tamu na za kumtakia maisha marefu.

Wengine walimsherehekea kama shujaa wa ukombozi wa uhuru wa pili miaka ya 90 huku wengine wakimtaka kiongozi huyo wa muda mrefu akiwa upinzani kama mtetezi wa wanyonge.

Hizi hapa ni baadhi ya jumbe za kumsherehekea na kumtakia heri njema anapoadhimisha miaka 79 duniani kutoka kwa Wakenya;

“Heri ya siku ya kuzaliwa Raila Odinga. Siku moja hata wasiokuthamini watasema neno la kukusifu. Baba akiwa na miaka 79 bado ana nguvu. Tunakupenda na umekuwa mwalimu mzuri kwa wengi. Siku moja tu, wote watasimulia hadithi nzuri kukuhusu,” Peter Salasyah.

“Heri ya siku ya kuzaliwa Rais wetu Rt. Mheshimiwa Raila Odinga anapofikisha umri wa miaka 79. Maisha marefu Rais Raila Odinga,” Okoko Jonathan.

“Heri ya Siku ya Kuzaliwa Rt Mheshimiwa Raila Odinga, Baba wa Taifa-Rais wa Watu. Angalia 79 imara hata baada ya miaka mingi ya kuzuiliwa na Moi,” Makau Wa Muli.

“Heri ya Siku ya Kuzaliwa Jakom Raila Odinga - Miaka 79 ni Dhahabu. Yako ni mazuri ya Dhahabu imepitia mengi, Pingu, Mapinduzi yaliyoshindikana, Kutoroka kwa Siri, Mateso, Hasara na Ushindi wa Kisiasa, Mawe, Mabomu ya machozi, Nguvu na vyote vinavyohusika kuwa Dhahabu! Natumai kusoma kumbukumbu zako siku moja!” UDAPartyKe.

“Raila Odinga akiwa na umri wa miaka 79 anaonekana mdogo zaidi kuliko Zakayo na Omuhana wa Hannah akiwa na miaka 57 na 63 mtawalia. Nini siri? Heri ya kuzaliwa @RailaOdinga, BABA wa DEMOKRASIA na UGAWAJI!” Joseph.

 Una ujumbe upi kwa kinara wa ODM leo hii anaposhereheka kuongeza mwaka mwingine?