Mtandao wa X waruhusu watumiaji kuweka maudhui ya watu wazima

Mtandao wa X almaarufu twitter umewaruhusu watumiaji kuweka maudhui ya watu wakubwa ila lazima waweke onyo kwa walio na umri wa chini ya miaka 18

Muhtasari

•Uchapishaji wa maudhui ya watu wazima ni rasmi ndani ya sheria mpya za Elon Musk mradi uwe na lebo na hauonyeshwi kwa uwazi.

•Takriban asilimia 13 ya machapisho ya  maudhui ya watu wazima mwaka wa 2022 yaliwekwa.

Jukwaa la mtandao wa kijamii X limeweka wazi kuwa sasa litaruhusu rasmi watu kuonyesha na kuweka maudhui ya watu wazima.

Maudhui ya watu wazima  yamekuwepo kwenye Twitter kwa miaka mingi na  tofauti na Facebook au Instagram haikupigwa marufuku kamwe hata kabla ya kuchukua madaraka kwa Elon Musk mwishoni mwa 2022.

Mwongozo mpya, ulioripotiwa kwa mara ya kwanza na Tech Crunch siku ya Jumatatu, unaruhusu watumiaji kwa uwazi kuweka maudhui ya watu wazima  mradi tu yanatolewa na kusambazwa  kwa watu wazima.

Chini ya sera mpya, uchapishaji wa maudhui ya watu wazima ni rasmi ndani ya sheria mradi uwe na lebo na hauonyeshwi kwa uwazi, kama vile katika picha za wasifu au mabango ya akaunti.

Akaunti ambazo huchapisha maudhui ya watu wazima mara kwa mara zitahitajika kutia alama kiotomatiki machapisho ya picha na video zao kama maudhui nyeti.

"Tunaamini kuwa watumiaji wanapaswa kuwa na uwezo wa kuunda, kusambaza, na kutumia nyenzo zinazohusiana na mandhari ya ngono mradi tu yanatolewa na kusambazwa kwa makubaliano. Usemi wa ngono,unaoonekana au unaoandikwa, unaweza kuwa njia halali ya kujieleza kwa kisanii." Ukurasa wa X kuhusu sera za "maudhui ya watu wazima" ulisomeka.

Aidha maudhui ya watu wazima  yatapigwa marufuku kwa watumiaji wanaotambuliwa kuwa watoto au watumiaji wazima ambao watachagua kutoyatazama.