Polisi waripotiwa kumuachilia kasisi aliyekamatwa na mwanafunzi ndani ya loji

Mwanafunzi alisema kasisi alimchukua nje ya lango la shule yake alipokuwa akielekea nyumbani na kumpeleka kwa pikipiki akiahidi kumnunulia vinywaji kabla ya kuhama hadi kwenye nyumba ya kulala wageni.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kasana kilichopo Kabwohe wilayani Sheema nchini Uganda wanakabiliwa na uchunguzi wa kumwachilia kiongozi wa kanisa waliyemkamata akiwa na mwanafunzi wa kike kwenye nyumba ya kulala wageni.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Naibu Mkuu wa Wilaya ya Sheema anasema askari polisi watakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kumwachilia huru mtu anayeweza kuwa na hatia ya unajisi.

Maafisa hao wa polisi walimkamata mhubiri katika Kanisa la Kitojo la Uganda huko Bikungu Archdeaconry huko West Ankole, akiwa kwenye loji na mwanafunzi siku chache zilizopita.

Mwathiriwa ambaye majina yake yamehifadhiwa, alisema kiongozi huyo wa kanisa alijilazimisha kwake.

 Alisema alimchukua nje ya lango la shule yake alipokuwa akielekea nyumbani na kumpeleka kwa pikipiki akiahidi kumnunulia vinywaji kabla ya kuhama hadi kwenye nyumba ya kulala wageni.

Wakristo katika eneo hilo walikuwa wamelalamika kwa muda mrefu kuhusu mhubiri huyo, na walipomwona akiwa na msichana huyo, waliwafuata hadi kwenye nyumba ya kulala wageni na kuwajulisha polisi.

Hata hivyo, Muhumuza aliachiliwa kwa dhamana ya polisi muda mfupi baada ya kukamatwa, jambo ambalo liliwakasirisha wakazi