' Rudisha mswada wa fedha bungeni,' Sonko amshauri Rais Ruto

Alibainisha kuwa mswada huo ulikuwa na kauli kadhaa ambazo hazitawahusu Wakenya.

Muhtasari
  • Katika taarifa yake kwenye mtandao wake wa kijamii, Sonko alimtaka Rais Ruto kurudisha mswada huo bungeni, akisema maoni ya Wakenya wanaoupinga yanafaa kusikilizwa.
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amemshauri Rais William Ruto kufikiria upya kutia saini Mswada tata wa Fedha wa 2024 ambao umezua taharuki kubwa miongoni mwa baadhi ya Wakenya.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wake wa kijamii, Sonko alimtaka Rais Ruto kurudisha mswada huo bungeni, akisema maoni ya Wakenya wanaoupinga yanafaa kusikilizwa.

"Kasmall advise to my good friend His Excellency the President kama hii nchi iko ndani ya roho yako na ulibeba bibilia pale Kasarani ukasema utatulinda sisi wakenya kupitia the Kenyan Constitution than return the Finance Bill 2024 back to the sender huko bungeni."

Sonko, ambaye alituma ambulensi 7 zenye matabibu 21 kusaidia waandamanaji waliojeruhiwa, alisema maandamano yaliyoshuhudiwa nchini yalivutia makundi kadhaa ya watu wakiwemo watoto wa matajiri.

Alibainisha kuwa wengi wao waliruhusiwa na wazazi wao kushiriki katika maandamano hayo.

"Watoto wa kiume wa watu mashuhuri akiwemo mwanangu katika Kaunti ya Kwale, na mtoto wa Askofu Mkuu Jackson Ole Sapit, miongoni mwa wengine, walijiunga na maandamano hayo. Hii inapaswa kukuambia kuwa si biashara kama kawaida," Sonko alisema.

Hapo awali, Sonko alikuwa ameshauri serikali kuwasikiliza wananchi kabla ya kuwasilisha mswada huo na kushughulikia ubomoaji Nairobi kwa amani.

Alibainisha kuwa mswada huo ulikuwa na kauli kadhaa ambazo hazitawahusu Wakenya.

Maandamano ya Jumanne ya kupinga muswada wa sheria ya fedha yalishuhudia nchi ikishuhudia matukio ya machafuko.