Mwanamume ajiingiza samaki mwenye urefu wa inchi 26 kwenye shimo lake la haja kubwa

Muhtasari

• Walimkuta samaki huyo amejaribu kutafuna njia yake ya haja kubwa kwa kung'ata ukuta wa utumbo wake mkubwa.

Samaki aliyeingizwa kwenye haja kubwa ya binadamu.
Samaki aliyeingizwa kwenye haja kubwa ya binadamu.
Image: HISANI

Mwanamume mmoja ambaye alijiingiza kiumbe wa baharini kwenye nja yake ya kutolea haja kubwa alijipata pabaya baada ya kiumbe huyo mwenye meno makali kuanza kung’ata kuta za utumbo wake akitafuta njia ya kutoka nje.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwenye jarida la New York Post, madaktari nchini Vietnam waligundua kificho chenye urefu wa inchi 26 katika vipimo vya X-ray vilivyochukuliwa ili kutambua sababu ya maumivu yake mnamo Julai 27.

Walimkuta samaki huyo amejaribu kutafuna njia yake ya haja kubwa kwa kung'ata ukuta wa utumbo wake mkubwa.

Inaarifiwa kwamba kijana huyo alimsukuma samaki kwenye njia yake ya kutolea haja kubwa kwa kutumia tunda la limau ambalo pia lilipatikana kwenye njia yake hivyo kufanya shughuli ya kumtoa samaki kuwa pevu.

Madaktari wa upasuaji walilazimika kumkata tumboni ili kutoa samaki kwa kutumia nguvu, huku picha za tumbo zikimuonyesha kiumbe huyo kwenye meza ya upasuaji.

Madaktari walirudisha limau chini kupitia njia ya haja kubwa hadi ikatoka kabla ya kushona tundu kwenye utumbo wake na kusafisha kinyesi kilichovuja.

Madaktari wanasema angekufa bila matibabu na atalazimika kuishi na mfuko wa colostomy maisha yake yote.