Kinyua na baraza la usalama nchini waamua kutoa ilani baada ya ghasia za Murang’a

Muhtasari
  •  Baraza la kitaifa la usalama latoa ilani kuhusu ghasia katika mikutano 
  • Kinyua awashtumu wanasiasa kwa kuwachochea vijana 
  • Agizo linajiri baada ya ghasia kutokea katika mkutano wa Ruto ,Murang'a 

 

Joseph Kinyua

 

 

  Mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua  ameagiza kwamba mikutano yote ya kisiasa ifanywe kwa mujibu wa sheria ya  kuandaa mikutano nawatakaokiuka sheria hiyo wataadhibiwa 

 

" Mtu yeyote anayeanda mkutano anafaa kumjulisha  OCS wa kituo cha polisi  siku tatu kabla ya mkutano huo’

 Akizungumza katika  kikao na wanahabari Kinyua amesema  wanasiasa wanawachochea wananchi na kuwapa itikadi kali .

"... Hakikisha unakuwepo wakati wa mkutano mzima na uwasaidie polisi kudumisha  sheria na usalama’ agizo lake limesema

 

Mbona kampeini zimeanza mapema? Wakenya tunasahau haraka? #PodiyaYusufJuma#YusufJuma#UchaguziKenya2022 Shirikiana,Wasiliana,Ungana au tangamana na Yusuf Juma Facebook:Yusuf Juma/Yusuf Juma-Kenya Instagram:@yusufjumaofficial Twitter:@YusufJumaKenya Email:yusufjuma86@gmail.com

 Kikao cha Kinyua na wandishi wa habari kinajiri baada ya ghasia kushuhudiwa huko  Murang’a katika hafla ya naibu wa rais william ruto ambapo watu wawili waliuawa katika machafuko .

Kinyua  amewahimiza wakenya kumripoti mtu yeyote anayetoa matamshi ya kuzua uhasama miongoni mwa wakenya .

 Pia amesema vyombo vya habari vitawajibikia kila vinavyochapishwa  endapo vitakuwa na hotuba za chuki .

 Siku ya jumapili makundi hasimu ya kisiasa ya tanga tanga na kieweke yalikabiliana huko Kenol katika kaunti ya Muranga  na kusaabisha umwagikaji wa damu pamoja na uharibifu .

 

 Uamuzi wa kinyua huenda ukakosolewa vikali na washirika wa naibu wa rais William Ruto ambao huenda watachukulia agizo hilo kama njia ya kuwazuia kuendelea  na msururu wa mikutano ya  hadhara kote nchini .