Watu 5 wafariki huku 321 wakipatikana na Covid 19

Muhtasari

 

  •  Nairobi inaongoza kwa visa 109
  • Watu watano wameaga dunia leo na kufikisha idadi ya walioangamizwa na corona hadi sasa kuwa 748
  • Watu 4328 wamepona  ugonjwa huo 

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

 

 Watu 321 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 4342 kupimwa katika saa 24 zilizopita .  Jumla ya visa hivyo nchini sasa ni 39,907  ilhali sampuli zilizopimwa sasa ni 569,678 .

 Kati ya visa hivyo vipya 309 ni wakenya na 12 i raia wa kigeni .Mgonjwa wa umri wa chini  ni mtoto wa miezi tisa ilhali wa umri wa juu ana umri wa miaka 88 . Nairobi inaongoza kwa visa 109 ,Nakuru ina visa 37 ,Trans Nzoia ina visa 32 , Mombasa ina visa 31 ,Kisumu ina 16,Narok 16,Kisii 15, Uasin Gishu 15 ,Meru 9,Kilifi 8, Kajiado 4,Laikipia 5,Kericho 3,Machakos 2, na Migori,Bomet ,Homabay,Nandi,Tharaka Nithi na Nyandarua zina kisa moja kila moja .

 

 Leo watu 4,328 wamepona ugonjwa huo na kufikisha jumla ya idadi ya walipona corona nchini kuwa  31,659. Hata hivyo watu 5 wameaga dunia na kufikisha idadi ya walioangamizwa na corona kuwa 748