Watu 3 wafariki huku visa 271 vipya vya covid 19 vikiripotiwa

Muhtasari

 

  •  Watu watatu wameaga dunia na kufikisha 751 walioangamizwa na Corona 
  • visa hivyo sasa vimefikia 40,178 tangu kisa cha kwanza kuripotiwa mwezi machi 

 

CAS wa Afya Rashid Aman

 Kenya siku ya alhamisi ilisajili visa vipya 271 vya corona  na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa 40,178  katibu mwandamizi wa wizara ya Afya Rashid Aman amethibitisha.

 Visa hivyo ni kutoka sampuli 5,034 zilizopimwa katika saa 24 zilziopita. Watu 242 ni wakenya huku 29 wakiwa raia wa kigeni. Idadi ya walioaga dunia kwa ajili ya ugonjwa huo imefikia 751 baada ya watu watatu kuaga dunia.

 Akizungumza katika kikao cha kutoa takwimu hizo huko Trans Nzoia Aman amesema mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali aliye na umri wa juu ana miaka 83.

 

 Watu wengine 51 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 31,710 idadi ya waliopona corona nchini.

Nairobi inazidi kuongoza kwa idadi ya juu ya visa 81 leo ikifuatwa na Mombasa 58, Turkana 16, Kisumu 15, Garissa 15, Kiambu 13, Kisii 10 Laikipia 8, Uasin Gishu 5, Nyamira 4, Kwale 2 na Meru 1