Raila Tosha! Wazee 500 kutoka jamii ya Kikiyu kumwidhinisha Odinga kuwa rais

Muhtasari

 

  •  Odinga hajatangaza iwapo atagombea urais lakini kila hatua zinazochokuliwa zinaashiria atakuwa kwenye debe 
  • Mkutano wa pili utanyika mwisho wa mwezi huu Nyeri wakati wazee wa Jamii ya Luo watakapowazuru wenzao wa Kikuyu 
  •  Pengo la tofauti ya kati ya Uhuru na naibu wake Ruto linazidi kuongezeka kila uchao 

 

 

Raila Odinga

 

Mamia ya wazee kutoka jamii ya kikuyu ,ngome ya kisiasa ya rais Uhuru Kenyatta   watamwidhinisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwania urais mwaka wa 2022 .

 Hafla hiyo itafanyika wikendi hii katika  boma la Odinga huko Bondo  na Zaidi ya wazee 500 wataifanya ziara hiyo ya kihistoria hadi nyanza kwa  azimio hilo .

 
 

 Mkutano huo  sasa I ishahara tosha ya jukumu la watu wenye ushawishi mkubw akatika Ikulu kumpiga jeki Raila kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022  baada ya kudhihirika wazi kwamba  wamekataa kumuunga mkono naibu wa rais William Ruto ambaye Uhuru aliahidi kumsaidia kuchukua hatamu atakapostaafu .

 Licha ya Raila kutotangaza iwapo atawania urais ,washirika w akaribu wa rais na wenye ushawishi wanaamini kwamba ni Odinga  pekee ndiye anayeweza kumzuia Ruto kuchukua hatamu katika uchaguzi mkuu ujao .

 “ Wakati wa mkutano huo Wazee watasema kwa kauli moja kwamba watamuunga mkono Odinga kugombea urais’ duru zimearifu .

  Baraza la wazee kutoka jamii ya Waluo na wabunge  kutoka ngome ya Odinga watahudhuria hafla hiyo . Baada ya mkutano wa Bondo  kundi la wazee kutoka jamii ya Waluo pia litachaguliwa kwa awamu ya pili ya mkutano  katika kaunti ya Nyeri tarehe 30 mwezi huu .

 Kakake mkubwa Raila  Oburu Odinga ambaye pia ni mbunge wa jumuiya ya afrika mashariki  amesema matayarishi yamefanywa kuwapokea wageni hao .

 “ Mgeni anapokuja kukutembelea ,unangoja ili kusikiliza ujumbe wake .huwezi kuweka ajenda ya ziara yake’ amesema Oburu

Siku ya jumamosi rais Kenyatta na bwana Odinga watahudhuria  hafla ya maombi ya madhehebu mbali mbali katika Ikulu ya Nairobi .

 
 

 Wadadisi wa kisiasa wanasema hatua ya kumwidhinisha Odinga yaonekana ni mpango wa  kusababisha mirengo  na kubadili dhana a wengi kuhusu siasa za urithi  huku  kila mgombeaji mkuu wa urais akimea mate kura za eneo la Mlima Kenya .

 Jamii hizo mbili zimekuwa katikati ya kila malumbano ya kisiasa  tangu Kenya ilipojinyakulia uhuru . Hata hivyo jamii hizo zimewai kushirikiana wakati Kenya ilipokuwa ikipigania uhuru  Mzee Jomo Kenyatta alipokuwa rais wa kwanza na wakati  Bwana Odinga alipomuunga mkono Mwai Kibaki kushinda urais mwaka wa 2002.

 Siku ya alhamisi mwenyekiti wa baraza la wazee wa Kikuyu Wachira Kiago  alithibitisha kwamba watasafari kwenda Bondo .