Sampuli 6,872 Zimepimwa

Watu 5 wafariki huku 538 wakipatikana na corona

Wanaume ni 430 ilhali wanawake ni 108 waliopatikana na corona

Muhtasari

 

  •  Watu 5 wamega dunia leo na kufikisha 760 walioangamizwa na Corona 
  • Watu 538 wapatikana na corona 
  • Nairobi inaongoza kwa visa 157 

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Kenya leo imesajili visa 538 vya corona  baada ya sampuli 6,872 kupimwa katika saa 24 zilizopita Idadi hiyo sasa inafiisha jumla ya visa vya corona nchini kuwa 41,158.Kutoka visa hvyo 496 ni vya wakenya ilhali 42 ni vya raia wa kigeni . Wanaume ni 430 ilhali  wanawake ni 108 .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 85 .

Nairobi inaongoza kwa visa vingi ikiwa na 157, Bungoma 118,Nakuru 48,Turkana 41,Mombasa 33,Kilifi 31,Uasin Gishu 61 ,Kisumu 13,Kisii 12,Meru 12,Garissa 9,Transnzoia 9,Narok 8,Kiambu 8,Kakamega 6,Isiolo 4,Kwale 3,Nyamira 2,Kitui 2,Migori 2,Busia  1,Elgeyo Marakwet 1 na Marsabiti 1

Leo watu 61 wamepona ugonjwa huo  na kufikisha jumla ya waliopona corona nchini kuwa 30,937 .Hata hivyo watu 5 wameaga dunia na kuzidisha idadi ya waliofariki kutokana na corona hadi 760 .