Watu 4 waaga dunia huku visa vipya 442 vikiripotiwa

Muhtasari

•Visa vipya leo ni 442
•Watu 4 zaidi wameaga dunia leo
•Nakuru inaongoza kwa mara ya kwanza leo kwa visa 94

CAS wa Afya Rashid Aman
Image: hisani

 

Kenya leo imesajili visa vipya 442 vya corona na kufikisha jumla ya visa hivyo kuwa 40,620 ,katibu wa utawala wa afya Rashin Aman amethibitisha .

Idadi hiyo ni kutoka sampuli 5,327 zilizopimwakatika saa 24 zilizopita . Kutoka visa hivyo 419 ni vya wakenya ilhali 23 ni vya raia wa kigeni .idadi ya sampuli zilizopimwa sasa ni 580,039

Idadi ya watu waliofariki kwa ajili ya ugonjwa huo imeongezeka hadi 755 baada ya watu wanne zaidi kuaga dunia . Akizungumza huko Uasin Gishu Aman amesema mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miaka 3 ilhali wa umri wa juu ana miaka 86 .

Watu wengine 166 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 30,876 waliopona ugonjwa huo . Kwa mara ya kwanza kaunti ya Nakuru inaongoza kwa visa hivyo baada ya kusajili visa 94 . kaunti nyingine ni;Nairobi 80, Mombasa 47, Embu 20, Kisumu 20, Meru 15, Garissa 12, Kajiado 11, Kericho 10, Kwale 2 na Bungoma 1.