Obado ananadai kuwa mshirika wa karibu wa DP Ruto

Obado amrai Raila kumlinda dhidi ya ‘Jeshi lake’

Odinga aahidi kuwaunganisha viongozi wa Migori

Muhtasari

 

  •  Obado  amekuwa akishambuliwa na viongozi wa ODM 
  •   Kumekuwa na jaribio la chama cha ODM kumfurusha Obado kama gavana 

 

Okoth obado
Gavana wa Migori Okoth Obado Okoth obado

 Gavana wa Migori Okoth Obado  ametoa ombi kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga kumkinga dhidi ya kushambuliwa na washirika wa karibu wa Odinga

 Ingawaje  hoja ya kumwondoa Obado afisini imeondolewa ,gavana huo amejikuta ametengwa katika wandani wa karibu wa Bwana Odinga huku akidaiwa kuwa karibu na naibu wa rais William Ruto .

 “ Nataka kukupa hakikisho kwamba nakuunga mkono kikamilifu .watu wamekuwa wakija kwako wakizungumza  na najua wanasambaza uvumi’ Gavana huyo amesema

Obado  amesema kila mtu ana maoni yake lakini hawafai kuambaza uvumi kumhusu  akisema kwamba kaunti ya Migori imekuwa aikiunga mkono ajenda ya chama cha ODM .

 Alikuwa akizungumza siku ya ijumaa wakati wa mazishi ya  Peter Sirawa babake mbunge wa Awendo  Walter Owino , na Raila pia alihudhuria mazishi hayo

 Alipozungumza ,Odinga alionekana kupuuza ombi la Obado lakini alisema kwamba kaunti ya Migori imegawanyika ,jambo alilosema sio zuri hasa uchaguzi wa 2022 unaponukia ,

 “ Hatufai kuzungumza kwa njia hii tunapoelekea 2022.Nitawaunganisha viongozi wa Migori hivi karibuni’ Alisema Odinga