Jerusalema

Kimunya, Mbadi wawaongoza wenzao katika densi ya 'Jerusalema'(Picha)

Wabunge nao hawajaachwa nyuma

Muhtasari
  •  Watu wengi  wamefanya shindano la kuucheza wimbo huo 
  • Kote duniani wimbo huo umetawala kumbi zote za video na densi 

 

 

   Kiongozi wa walio wengi bungeni Amos Kimunya na mwenzake wa walio wachache John Mbadi siku ya jumatano wamewaongoza  wabunge  kufanya densi ya wimbo maarufu wa Jerusalema.

 

 Wabunge waliunda foleni mbili sako kwa bako ili kuifanya densi hiyo  katika majengo ya bunge huku  wakijaribu kufuata mfano wa miondoko na unenguaji ambao maelfu ya watu wamefanya kote duniani tangu  shindano hilo la kudensi kuanza.

Kimunya  na Mbadi  waliwasisimua wenzao kwa weledi wao kufanya densi hiyo  huku wakishangiliwa .

 Wabunge wamekuwa wakifanya mazoezi ya kuweza kufanikisha densi hiyo kwa siku mbili. Kimunya  amesema ni muhimu kwa viongozi pia kuwa sehemu ya vugu vugu kama hilo la kijamii wakati huu mgumu.

 Wimbo wa Jerusalema umepigwa jeki na idhinisho kutoka kwa marais, makasisi na makundi mbali mbali ya watu, vikosi vya usalama na hata kampuni nyingi kote duniani.